Mapema wiki iliyopita Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango ilitembelea miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali
nchini ili kukagua utekelezaji wake. Miradi hiyo ni pamoja na Kituo cha
kuzalisha samaki Morogoro, Skimu ya Umwagiliaji Iringa vijijini, Maghala ya
COWABAMA Iringa Vijijini, Ujenzi wa Barabara ya Iringa – Dodoma, Bwawa la
Mtera, Ujenzi wa Barabara ya Manyoni – Itigi, utandikaji wa Reli eneo kati ya Kitaraka
na Malongwe, Shamba la Kitengule, One Stop Border Post Mutukula, Mkongo wa
Taifa Mutukula na Upanuzi wa mradi wa maji safi, Bomba Kuu la Ziwa Victoria.
Katika
kufanikisha uratibu wa miradi ya maendeleo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
hufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuzielekeza
Wizara zinazotekeleza miradi kuwasilisha taarifa za utekelezaji kila robo
mwaka. Aidha, Tume ya Mipango hutembelea miradi ya maendeleo kuona hali halisi
ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na kubaini mafanikio na changamoto na hatimaye
kutoa ushauri katika ngazi husika kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto
hizo.
Moja ya Majukumu
ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ni kuratibu utekelezaji wa miradi ya
maendeleo ya Kitaifa ya Kimkakati, Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa (MMS) na
miradi mingine muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa. Miradi imeainishwa katika
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16) na ile ya
Matokeo Makubwa Sasa iliyoibuliwa katika mfumo wa kimaabara.
Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri (wa nne kulia), Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari
Abdallah (wa kwanza kushoto) na maafisa kutoka
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango pamoja na wataalam wa Mradi wa Kituo cha Kuzalisha Samaki kilichopo Kingolwira Mkoani Morogoro wakiangalia sehemu maalum ya kukuzia vifaranga vya samaki baada ya kutotoleshwa.
Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Bibi. Florence Mwanri (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi
wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari
Abdallah (wa kwanza kulia) pamoja na maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango wakipata maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Iringa – Dodoma, hatua ulipofikia na changamoto zilizopo kutoka kwa Mtaalamu Elekezi wa mradi Bw.Robin de Kock (mwenye kofia).
No comments:
Post a Comment