‘Je
Tuseme Jiwe walilolikataa waashi, limekuwa Jiwe Kuu la Pembeni?’
Na
Bryceson Mathias
KATIKA gazeti la Tanzania Daima, Toleo Na.3729 Jumatano, Februari 18, 2015 kwenye
Ukurasa wa Saba, lenye kichwa cha Habari ‘Kinana ana Upendeleo kwa
Wagombea Urais CCM’!.
Kwenye
Makala hiyo, niliandika nikionesha kuwa, hata Mteule wa Chama cha Mapinduzi
(CCM), John Pombe Maghufuli, naye alianza Kampeni kabla ya wakati kama ilivyo
kwa waliotuhumiwa akiwemo, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyai
Lowassa.
Baada ya
Malalamiko ya Wananchi na Wadau kuhusu Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba,
kudaiwa ameanza Kampeni akijificha kwenye Pazia la nafasi yake ya
Kazi serikalini na Chama chake, CCM kupitia kwa Katibu, Abdulahman Kinana,
alimwandikia, Nchemba, kusimamisha Ziara zake za CCM mikoani.
Hali hiyo
haikulalamikiwa kwa Nchemba peke yake, lakini pia ilionesha Watia Nia wengi wa
Urais ndani ya CCM ambao kwa ujumla walikuwa nyadhifa kubwa serikalini
(Uwaziri), kwa namna moja au nyingine walitumia sana nafasi zao kufanya Kampeni
zinazodaiwa.
Katikati ya Januari 18, 2015, kwenye Mitandao ya Kijamii,
kuliwekwa Barua yenye Kumb. Na. CCM/OND/4 iliyokuwa ikienda kwa Naibu Katibu
Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba, iliyokuwa na kichwa cha habari ‘KUSITISHWA ZIARA’
Iliyosomeka hivi;
“Umekuwa ukifanya ziara nyingi katika Mikoa na Wilaya bila ya
ushirikishwaji kamili na Makao Makuu, Mikoa na Wilaya, na hasa Kamati za Siasa.
“Wewe pia umeonyesha kwa Kauli na Mienendo yako kujiandaa kugombea nafasi ya Urais kupitia CCM. Ziara hizi zina mwelekeo wa kampeni, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Chama.
“Nakuagiza kuzisitisha ziara zote. Iwapo utataka kufanya ziara
yoyote ya kichama, itabidi kwanza uniarifu na upate kibali changu. Nakuagiza
kutekeleza agzo hili mara moja” mwisho wa Nukuu.
Katika
ziara hizo, Mwigulu alipoulizwa alijitetea akisema, kama Naibu Katibu Mkuu wa
CCM, alikuwa akikagua Uhai wa Chama, na kutatua Kero Lukuki zinazowakabili
watendaji, kutokana na Malalamiko mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wananchi
katika maeneo yao.
Mbali ya
Watia Nia Sita wa Urais CCM akiwemo Lowassa, kupewa adhabu ya Kufungiwa Miezi
Sita kwa madai walianza Kampeni kabla, kwa mujibu wa Sheria, hata Magufuli naye
alikuwa ameanza harakati hizo kama walivyofanya wengine.
Ingawa,
baadhi ya watetezi wanadai alikuwa hajatia Nia lakini tayari alikwisha tajwa
kuwa mmoja wao, ingawa hakutaka kujionesha, lakini yeye aliachwa aendelee
kutumia Nafasi yake ya kukagua Miradi ya Barabara, Kuzifungua, ikiwemo Mikutano
na Semina za Watalaam, akihutubia wananchi nchi nzima.
Kama
mtakumbuka vizuri, Machi 16, 2015 Makamu wa Rais Dk.Mohamed Bilal, alipokagua
Mzani mpya na wa Kisasa kabisa Vigwaza, ambapo gari lisilozidisha litapima kwa
sekunde thelathini badala ya dakika mbili akiwa na Magufuli akitoa taarifa,
ilikuwa ni moja ya Turufu zake.
Kati ya
17-18 Mei, mwaka huu kwenye Semina za Watalaam wa Ujenzi (CPD) Mlimani City,
Magufuli pia alikuwa na Fursa ya kuwa na Makandarasi, Wahandisi, Wasanifu
Majengo nchini, ambapo semina hiyo iliyokuwa ifanyike Tanga, yeye kama Mkuu wa
Wizara, aliibadilisha ikafanyika Tanga. Hivyo nakataa mtu anaposema wengine
hawakufanya Kampeni mapema, tutoe haki, wote walifanya.
Kutokana
na kile kilichofanyika Dodoma wakati wa uteuzi wa Mgombea Urais wa kupeperusha
Bendera ya CCM dhidi ya Lowassa, ambapo yeye mwenyewe anasema, hakuamini kama
kilichofanywa na chama chake, kimefanywa na CMM iliyomlea, hapo ndipo naamini, Lowassa
aliipenda CCM isiyompenda isipokuwa Wanachama walimpenda.
Katika
hali hiyo, ndiyo maana wadau wanasema, huenda Lowassa aliipenda CCM
isiyompenda, kwa sababu, Turufu aliyotumia Magufuli kwamba anafanya Ukaguzi wa
Barabara na Miundo Mbinu, haikuishia hapo, pia alitumia Mikutano ya Watalaam wa
Mambo ya Ujenzi kujinadi, hivyo naye alianza Kampeni mapema kama wengine.
Lowassa
aliuenzi Upinzani au Laa?.
Wasomi na
Wadau wa Siasa, wamekuwa wakijiuliza maswali; Je, Lowassa kufikia
kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliuenzi upinzani?
Tunapotafuta majibu hayo, basi hebu tushirikiane kwa pamoja bila kudhani
alifanya hivyo kwa kuksa nafasi CCM.
Pamoja na
Lowassa kutajwa kwenye Orodha ya Aibu ya Mafisadi kule Temeke Mwembe Yanga,
hatukuwahi kusikia akilipiza Kisasi au kufanya Majibishano akipinga au
kulumbana na taarifa za Shutuma zilizoelekezwa kwake.
Licha ya
kuwepo majibishano mbalimbali Makali ndani ya Bunge kuwahusu Wapinzani,
hatukuwahi kusikia akisimama na kuwaponda Wapinzani kuburuzana kwa ubishi,
akiwararua au kuwagandamiza akikataa hoja zao.
Kwa muda
wote, Lowassa tangu ajiuzulu Uwaziri Mkuu, alikaa kimya kama Mtu
anayetunga Sheria, na kwa nyakati tofauti vyombo vya habari na Wananchi
walishangaa sana na ukimya wake huo, na kutafsirika kwa mambo mengi dhidi
yake.
Kwa
mtazamo huo, ndipo ninapohitimisha Mjala wa Swali la Lowassa aliuenzi Upinzani
au Laa? Mimi nasema aliuenzi, maana kwa maelezo machache ya awali hapo juu,
inaonesha hata siku moja hakuwahi, kuwasema vibaya wapinzani wala kuwang’ong’a
au kuharibu mipango yao, hivyo aliuenzi upinzani! .
Na kwa
namna hiyo, sioni kama kuna mikwaruzo yoyote ambayo, Lowassa inaweza kumsumbua
atakapokuwa ndani ya Chadema, ingawa kuna baadhi ya watu wanaweza kupata taabu
kutokana na walivyomtafsiri au kumsema, jambo ambalo wanaweza kusameheana tu
aana ni katika vita ya siasa!.
Sasa hivi
kumetokea maneno na minong’ono mingi kwamba, Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt.
Wallboard Slaa, amejiuzulu nafasi yake na amekabidhi Kadi ya Chama hicho, na
kwamba eti anakwenda Chama cha ACT-Wazalendo akiwemo, John Mnyika, kwa
kuwa hawaridhiki kupokewa kwa Lowassa.
Bado
sipingani wala kukubali Taarifa za vyombo vya habari hivyo kwenye gazeti lake
la kila siku la Ijumaa na Jumamosi hivi karibuni, ila nakubali kutokukubaliana.
Nasema hivyo kwa sababu, yote yanaweza kutokea kama vile Lowassa ilivyotokea
kuhamia Chadema.
Ninachofahamu
mimi, Slaa na Mnyika waliipenda Chadema na Wanachama wake, ambao nao
waliwapenda, kama kweli, Slaa na Mnyika wanaipenda Tanzania, na wanaumizwa na
Adha wanayopata Watanzania kila kukicha, kiasi wanakosa hata Mulo wa siku moja,
kwa busara zao hawezi kushindwa kujitokezaw auambie Umma ukweli, maana wao ni
wa kweli!
Akifika
mahali penye hisia za namna hiyo, huo ni Mshindo na Mwanguko wa Tembo kisimani
ambapo, Samaki wadogo na Wakubwa, Chura na wanyama wengine majini, watakufa
kutokana na Uzito wa Mnyama huyo.
Ninachosema,
‘Mungu Ibariki Tanzania………………………”
0715933308
No comments:
Post a Comment