Na Bryceson Mathias, Ruaha-Kilosa
BAADA ya kuwepo Mizengwe
na Mamluki toka nje ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya
Ruaha Kilombero kutaka kuvuruga Uchaguzi wa Mgombea wa Udiwani, hatimae Mshindi
wa Matokeo ya Mnyukano wa Uchaguzi huo, sasa yamewekwa Hadharani.
Katibu wa Chadema Kata ya Ruaha, Joramu Zacharia, alimtaja Isaack
Maliwa, kuwa ndiye Mshindi kwa kujikusanyia Kura (43), akiwashinda, George Banda (40),
Ally Mponda (6), Mathias Luambano (4), Kilango Mshana (0) na Manji Mbando (0).
Uchaguzi huo uliwahusisha Wagombea Sita (6),
ambapo wapiga kura walikuwa 95, wakiwa ni Wajumbe toka katika Vijiji Vinne (4)
vya, Ruaha, Simbalembende, Nyanvisi na Kising’a, vikiwakilishwa na Wenyeviti wa
Vitongoji na wajumbe wa Baraza la Kata ya Ruaha.
Akiwashukuru Wajumbe
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilosa, Kamanda Libenaga, alisema Kata ya Ruaha
ndiyo yenye Chachu ya Mabadiliko, ambayo kwa sehemu kubwa itasaidia kupata
Ushindi wa Ubunge wa Jimbo la Mikuni kwa sababu ina watu wengi.
Mshindi wa Uchaguzi
huo, Maliwa, aliwashukuru Wapiga Kura wote, huku akikiri kuwa ulikuwa na
ushindani Mkubwa, ambapo alisema kama Chama kitaridhia na kumpitisha apeperushe
Bendera ya Chadema katika Uchaguzi huo, atashirikiana na Wagombea wote
kuhakikisha Wanapata Ushindi wa Kata ya Ruah na Jimbo la Mikumi.
Hata hivyo, Maliwa aliahidi,
“Kama Chadema kitampisha Kugombea Uchaguzi wa Kata ya Ruaha, Mshindani wake
aliyemfuatia, Banda, atakuwa Kampeni Meneja wake, ili kwa Umoja na Mshikamano
wao, ulete Mabadiliko Makubwa zaidi”.alisema Maliwa.
Kauli hiyo iliungwa
Mkono na Mshindani wake Banda, ambaye bila Kinyongo huku wakikumbatiana, alikubali kushirikiana na Mshindi huyo, endapo
atapitishwa na Chama chao, ambapo Wajumbe na Wasimamizi wa Uchaguzi huo,
walipendezwa na Mshikamano na Umoja ulioonyeshwa.
No comments:
Post a Comment