Na Bryceson Mathias, Morogoro
UCHAGUZI wa Waandishi wa Mkoa wa Morogoro, umempa Ushindi Mwandishi Mkongwe wa Startv, Nickson Mkilanya, ambaye amechaguliwa kwa Kura nyingi za Ndiyo na hivyo Mwenyekiti Mpya wa Klabu ya Waandishi ya Morogoro, Moro Press Club, huku Kura Tatu zikisema hapana.
Katika uchaguzi huo Mwandishi wa Magazeti ya Nipashe na The Guardian, Ashton Balaigwa kuwa Makamu Mwenyekiti, huku akimtupa kwa mbali Afisa Habari na Mahusiano wa Wilaya ya Mvomero, Gerald Nkamia.
Aidha Mwandishi wa Radio Ukweli,Morogoro, John Kidasi, aliinuka Kidedea akishinda na kuwa Katibu Mkuu Mtendaji wa Moro Press, ambapo nafasi ya Usaidizi wa Kaimu Katibu Mkuu ilikwenda kwa Jimmy Mengele, Mwandishi wa Channel Ten.
Naye, Merina Robert, alinyakua nafasi ya Mwekahazina Mkuu wa Moro Press, ambapo nafasi ya Msaidizi wa Mwekahazina, ilikwenda kwa Mwandishi wa Magazeti ya Habari Leo, Christina Haule, huku Wajumbe watatu, Severin Blasio, wa Majira, Fadhiri Rashidi, na Fitina Haule walipita bila kupingwa kwa sababu hawakuwa na washindani, baada ya mmoja wao wa Nne kukosa Sifa.
Baada ya Uchaguzi, huo uliosimamiwa na Viongozi Baraza la Habari, Afisa Programu Udhibiti na Uwajibikaji wa Vyombo vya Habari (MCT), Paulo Mallimbe, aliwashuru walioshinda, huku akimtaja Mwenyekiti, Mkilanya kwamba inaonekana anakubaliwa maana amezoa Kura zote isipokuwa Tatu (3).
Akishukuru wapiga Kura, Mkilanya aliahidi kurejesha Umoja wa Waandishi unaoashiria kutoweka miongoni mwa Waandishi Morogoro, ambapo aliagiza kvunjwa Makundi na kwamba kilichobakia ni Kazi, huku akiahidi Moro Press kuwa na Ofisi yake binafsi katika Uongozi wake.
Hata hivyo uchaguzi huo nusura uingie Dosari, pale wanachama wapya walipotaka kupiga Kura kabla ya kujadiliwa na kukubalika na Mkutano Mkuu kama ilivyo Katiba ya Moro Press Club, ambapo Wajumbe wa Mkutano Mkuu waliridhia Wanachama wapya wote wapishi uchaguzi ufanyike kwanza!
Mapema Mkutano huo ulifunguliwa na Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Nchini (TASAF), Ladislaus Mwamanga, ambaye alisema, TSAF inawapenda Waandishi kwa Kazi yao, hivyo aliwataka kuandika habari za Ukweli na Uhakika na kuwaahidi TASAF ina fungu la Mafunzo kna Semina kwa Waandishi.
No comments:
Post a Comment