Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshinda (wa pili kushoto) akisistiza jambo wakati wa mkutano huo. Wengine pamoja nae ni
wajumbe kutoka Serikali ya Japan.
Na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango, pamoja na majukumu mengine, inajukumu pia la
kuratibu miradi ya maendeleo kwa ajili ya ufadhili wa serikali
ya Japan kila mwaka.
Maandalizi ya mwaka
huu yameshakamilika na mkutano wa majadiliano kati ya Serikali ya
Jamhuri ya
Muuungano ya Tanzania na Serikali ya Japan ulifanyika mwishoni mwa wiki
iliyopita katika Hotel ya Hyatt Regeny, The Kilimanjaro, Dar es Salaam.
Majadiliano hayo kwa upande wa Serikali ya Japan yaliongozwa na Bw.
Masaharu
Yoshinda, Balozi wa Japan nchini Tanzania, kwa upande wa Tanzania
yaliongozwa
na Mhandisi Happiness Mgalulla, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais,
Tume ya
Mipango.
Malengo ya mkutano huo ni kujua hatua iliyofikiwa katika
maombi ya ufadhili wa miradi ya maendeleo kutoka Serikali ya Japan kwa mwaka
2014/15, kuwasilisha miradi ya maendeleo kwa ajili ya ufadhili kwa mwaka
2015/16, kujadiliana changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi na
kupendekeza hatua za kuchukuliwa ili kuboresha ushirikiano baina ya Serikali
hizi mbili. Pia Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, iliwasilisha mawazo ya awali ya
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP II).
Wizara zilizoshiriki katika Mkutano huo ni pamoja na Ofisi Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na
Wizara ya Fedha.
Wizara zingine ni pamoja na Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ujenzi,
Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Chakula na Ushirika, Wizara ya
Mifugo na Mendeleo ya Uvuvi, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Maji na
Umwagiliaji, na Tume ya Mipango – Zanzibar.
Kwa upande wa Serikali ya Japani taasisi zilizohudhuria ni pamoja na
Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, JICA – Tanzania, Makao Makuu ya JICA- Japan
na Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan.
No comments:
Post a Comment