Na Bryceson Mathias, Mvomero-Morogoro
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetupilia
mbali pingamizi lililowekwa na mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Sadiq
Murad, dhidi ya Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Osward
Mlay, wa Jimbo la Mvomero, Morogoro.
Mchungaji Mlay
amekiri kuwekewa Pingamizi na Murad aktilia shaka Jina a Elimu yake, ambapo
Mchungaji Mlay amesemaalmelijibu na limetupiliwa Mbali na anaendelea na
Maandalizi ya kufungua Kampeni.
“Ni kweli niliwekewa Pingamizi na Mgombea
Mwenzangu (Murad) wa CCM, lakini nadhani
alikosa Uelewa, lakini nimelijibu Pingamizi lake na limetupiliwa mbali, na sasa
najiandaa kwenda Morogoro kwa maandalizi ya Kampeni.
“Naomba niombeani, kimsingi hatuna muda wa
kujadiliana na Watu ambao, Mungu amemwinua Musa aende kwa Farao, awatoa Watu
waende nchi ya Maziwa na Asali, amemwinua Yusuf, akaandae Chakula kwa Miaka
Saba ya Njaa inayokuja, halafu mtu anazuiamia, anazuia! Tusimkubali”.alisema
Mlay”.
Chma kimenichagua nipeperushe Bendera ya Chadema,
kwa hiyo katika hili, Wananchi na Wanachama wenye Uchungu wa Mateso
waliyofanyiwa na CCM kwa Miaka 50 ya Uhuru, ambapo haki za Wafanyakazi, Wafanyabiashara,
Wakulima na Wafugaji, zimekuwa zikiporwa, wajipange tuvuke Ng’ambo ya Mto.
Aidha aliwataka Wananchi, Viongozi wa Dini, akina
Baba, Wazee, akina Mama na Vijana wa Jimbo la Mvomero, wasiichezee nafasi hii
ambayo Mungu amewapa Wana Mvomero, wakabaki kuzunguka kwenye Mlima wa Seiri,
ila wageuke upande wa Kulia uliko Ukombozi wa Mungu.
‘Wana Mvomero, Mlivyozunguka Mlima huu (wa adha na dhuluma za CCM kwa Miaka 50 ya
Uhuru) Vyatosha, geukeni pande wa Kaskazini.”alisema Mchungaji
Mlay, akinukuu Maandiko Matakatifu ya Biblia, Kumbukumbu la Torati Sura ya Pili
2 Mstari wa Tatu(Kumb.2:3).
No comments:
Post a Comment