August 10, 2015

WAZIRI MKUU PINDA AWASHANGAA WANAOHAMA CHAMA BAADA YA KUSHINDWA

Na Emanuel Madafa, Mbeya
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mchakato wa kumpata mgombea wa  urais kupitia chama cha mapinduzi  (CCM) umekwenda vizuri hivyo kwa wale wale ambao hawakufikia malengo nivema wakakubali  matokeo kwani ilikuwa lazima  mmoja apatikane.
Amesema   busara nzuri ni kukubali matokeo hayo  badala ya kuhama chama kama walivyo fanya baadhi ya makada wengine wa chama hicho.
Waziri Mkuu Pinda ametoa kauli hiyo mkoani mbeya wakati akifunga maadhimisho ya sherehe  za wakulima Nanenane kwa mikoa ya kanda za nyanda za juu kusini katika viwanja vya John Mwakangale.

Amesema, katika mchakato wa kuomba nafasi ya urais wagombea walikuwa zaidi ya 40 lakini aliyekuwa akihitajika mmoja hivyo ni vema wengine ambao majina yao yaliondolewa kutokana na kutokidhi vigezo mbalimbali vya chama  wangekubali matokeo kuliko kuhama chama.
Amesema yeye kwa upande wake ameridhika na mchakato huo hivyo haoni sababu ya kuondoka  ndani chama  hicho kwani ndicho  chama kilicho mfikisha hapo alipofikia sasa nakutumikia nafasi hiyo ya uwaziri Mkuu kwa miaka 8  hadi anakoma utumishi wake.
Pinda amesema kama kuna mambo ya kusahishana atafanya hivyo akiwa ndani ya chama cha mapinduzi  kwani hata huko ambako wengine wamehamia hakuko salama na kunachangamoto nyingi hiyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kumchagua kiongozi bora atakaye wafikisha mahala pazuri.

Hata hivyo, aliwataka wanachama wa CCM  kutambua kuwa sera nzuri za vyma ndizo zitakazo saidia kuwashawishi watu kukikubali chama hivyo hakuna sababu ya kuhama zaidi ni kuziboresha sera zilizopo ili watu wazipende na kuzikubali
Katika hotuba yake waziri Mkuu Pinda amewataka viongoizi wa mikoa hiyo ya kanda za nyanda za juu kusini  kuhakikisha wanajikita katika kuwasaidia wakulima na wafugaji wadogo wadogo ili kuwainua kiuchumi badala ya kushughulika na wakulima wakubwa pekee.
Amesema uchumi wa Tanzania unakuwa lakini bado hauendani na hali hali ya maisha ya watanzania hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kupigana na hali ya umasikini  sanjali na kuondoa utofauti  ya aliye nacho na asiye nacho.
Hata hivyo waziri Mkuu Pinda amesema anajivunia katika kipindi cha utumishi ndani ya serikali ya rais kikwete  kwa kuweza kuinua sekta ya kilimo kwani nchi imeweza kupeleka tanni 500 za mahindi katika nchi jirani ya Ethiopia, Sudani tanni 500, Burundi tanni 500 , Malawi tanni 500 na nchi nyingine za jirani hivyo hii ni hatua kubwa sana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza wakati wa kilele cha Sikukuu ya Wakulima ya Nanenae mkoani Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza katika sherehe hizo za wakulima Nanenane Kanda ya Nyanda za juu kusini katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi zawadi kwa washindi wa manesho hayo katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Agost 8 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Pages