Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif
akizindua Maskani ya CCM ya Vijana wa Jimbo la Kiwani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba iliyopewa jina lake.
Balozi Seif akipandisha Bendera ya Maskani ya CCM
ya Vijana wa Kiwani Iliyopewa jina la Balozi Seif Maskani mara baada ya kuizindua rasmi katika sherehe iliyofanyika Jimboni humo.
Baadhi ya wanachama wa CCM na Wsananchi wa Kijiji
cha Kiwani Michakweni wakifuatilia Hotuba ya Balozi Seif hayupo
Pichani wakati wa uzinduzi wa Maskani ya Jina wa Kijiji hicho
iliyopewa jina lake.
Balozi Seif akisalimiana na Sheikh Faki Mohammed
Khamis ambae ni mlemavu asiyeona baada ya kusoma Quran Tukufu wakati wa uzinduzi wa Balozi Seif Maskani hapo Kiwani Wilaya ya Mkoani.
Vijana Zuhura na Safi wakighani utenzi murua uliotoa
burdani safi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Balozi Seif Maskani ya Vijana wa CCM wa Kijiji cha Kiwani Michakweni.
Vijana wa Maskani ya CCM ya Balozi Seif iliyopo
Kiwani wakitoa burdani ya nyimbo maalum iliyoanikiza katika uzinduzi wa Maskani yao waliyoamua kuipa jina la Balozi Seif Maskani.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Shaka
Hamdu Shaka akiwakumbusha Vijana wa Kiwani Michakweni kuelewa wajibu wao wa kuhakikisha CCM Inaendelea kushika dola kwa kuwapa ushindi wagombea wa Chama hicho.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya
CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wanachama wa CCM wa Jimbo la Kiwani mara baada ya kuizindua Balozi Seif Maskani ya Kijiji hicho.
Haiba ya Jengo la Balozi Seif Maskani liliopo
Kiwani Kichakweni lililojengwa kwa kuzingatia Utamaduni wa Visiwa vya Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha
Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi
amewaasa Wanachama wa Vyama vya
upinzani Kisiwani Pemba
kuacha kuendelea kukumbatia Viongozi ambao
tayari wameshaonyesha
muelekeo wa kutokubali kusimamia maendeleo yao
kwa zaidi ya miaka Ishirini
sasa.
Alitoa nasaha hizo wakati
akizungumza na Wanachama wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) na
Wananchi wa Kijiji cha Kiwani – Michakweni Jimbo
la Kiwani mara baada ya
kuizindua Rasmi Maskani ya Vijana wa CCM wa
Jimbo hilo iliyopewa Jina lake.
Balozi Seif alisema wakati wa
kuacha kudanganywa kwa sera na ahadi
zisizotekelezeka za Viongozi
hao wanaojali maslahi yao binafsi umefika
kwa wafuasi hao wa Upinzani na
badala yake wajiunge na Chama cha
Mainduzi kabla hawajaachwa njia
panda.
Alisema Gari la Chama cha
Mapinduzi hivi sasa bado linaruhusu
kupakiwa abiria wowote
watakaoamua kutoka vyama vya upinzani ambao
wanaonekana kuchoshwa na
vitendo vinavyoviza Maendeleo yao kwa kiindi
kirefu sasa.
Balozi Seif alielezea faraja
yake kutokana na Wananchi walio wengi
Kisiwani Pemba kuonyesha dalili
za kuchoshwa na hatimae kukataa
Viongozi wasiojali Maendeleo ya
Wananchi.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya
CCM Taifa alisema katika kuuzika upinzani
katika Uchaguzi Mkuu ujao wa
mfumo wa Vyama vingi vya Siasa
aliwakumbusha Wana CCM
waendelee kushikamana lengo likiwa ni kumaliza
upinzani huo usio na muelekeo
wa Maendeleo.
Amewapongeza Vijana hao wa
Balozi Seif Maskani wa Kiwani Michakweni
kwa uamuzi wao wa kujenga Jengo
lililozingatia Utamaduni wao na
kuwaahidi kusaidia kuiimarisha
katika kiwango kinacholingana na Chama
chenyewe.
Alisema msaada huo utakwenda
sambamba na kuzingatia mipango imara ya
kuwapatia Boti ya uvuvi
itakayowapa fursa ya kujiajiri wenyewe ili
waweze kukidhi mahitaji yao ya
Kimaisha.
Balozi Seif alieleza kwamba
tabia ya kukaa vijiweni hivi sasa imepitwa
na wakati kulingana na
mabadiliko ya mfumo wa Dunia uliopo hivi sasa
ambao unamkaba mwanaadamu
lazima afanye kazi.
Akitoa Taarifa fupi ya
Vijana hao wa Balozi Seif Maskani Mmmoja wa
Viongozi wa Maskani hiyo Ndugu
Mohammed Juma alisema Maskani hiyo
imeasisiwa Mwaka 2014 ikianza
na Wanachama 22 na hivi sasa imeongeza
wanachama na kufikia 36.
Nd. Mohammed alisema
kwamba Vijana hao wamejipanga kuwa Maskani ya
chuo cha Vijana katika
kuwafundisha sera za Chama cha Mapinduzi
pamoja na Itikadi zake
zitakazosaidia Vijana hao kuelewa Historia ya
Taifa hili lililojikomboa
kutokana na madhila ya wakoloni.
Vijana hao wa Balozi Seif
Maskani Kiwani Michakweni wameupongeza
Uongozi wa Serikali ya Wilaya
ya Mkoani kwa kuwahakikishia usalama
licha ya vitisho wanavyoendelea
kufanyiwa na wafuasi wa Upinzani kwa
uamuzi wao wa kuunga mkono
Chama cha Mapinduzi.
Naye akisalimia na Vijana hao
wa Balozi Seif Maskani ya Kiwanchi
Michakweni Mke wa Mjumbe huyo
wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mama Asha
Suleiman Iddi amewataka akina
Mama wa Kijiji na Jimbo hilo kuhakikisha
kwamba Viongozi
watakaowachaguwa wawe tayari kufanya nao kazi pamoja.
Mama Asha alisema wapo
viongozi wenye tabia ya kwenda Majimboni
kuomba kura na baadaye
kuwatelekeza Wananchi hao bila ya kujali kwa
vitendo vyao vya kutafuta
maslahi katika maeneo mengine vinawanyima
haki Wananchi wao.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar










No comments:
Post a Comment