Mbunge wa jimbo la Kilolo Bw Venance Mwamoto akikabidhi fedha akisi cha Tsh 500,000 kati ya Tsh milioni 1 alizoahidi kuchangia ukarabati wa darasa la chekechea kijiji cha Isele kata ya Ilula
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Bw Venance Mwamoto achangia kiasi cha Tsh milioni 1 kwa ajili ya kuwaunga mkono wananchi wake kijiji cha Isele kata ya Ilula wilaya ya Kilolo ambao wamejitolea kufanya ukarabati wa darasa la chekechea kwa lengo la kusogeza elimu kwa watoto kijijini hapo.
Huku akiwataka wananchi wote kuendelea kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ,shule na nyumba za walimu na kuwa serikali ya Rais Dr John Magufuli imefuta ada na michango na sio uchangiaji wa ujenzi .
Akikabidhi kiasi cha Tsh 500,000 kati ya Tsh milioni 1 ambayo amepanga kuwachangia wananchi hao leo mbunge huyo alisema kuwa baada ya kufika kuhamasisha wananchi kuchangia shughuli za kimaendeleo zikiwemo za elimu alikutana na changamoto ya ukosefu wa darasa la awali katika kijiji hicho na hivyo kuwahamasisha wananchi kuanza kutatua tatizo hilo.
Bw Mwamoto alisema kuwa baada ya kufika katika kijiji hicho uongozi wa kijiji ulimtembeza eneo hilo ambalo wananchi walikusudia kufanya ukarabati wa darasa kwa ajili ya wanafunzi wa chekechea na kuwa mahitaji yote pamoja na nguvu za wananchi ilikuwa ni Tsh milioni 2 na hivyo kulazimika kuchukua mzigo wa kuchangia pesa kiasi hicho cha Tsh milioni 1
" Kimsingi hali ya darasa lile haikunifurahisha hivyo niliwataka kufanya marekebisho ili watoto hao kuweza kusoma katika mazingira bora zaidi na hii pesa nimetoa kwa ajili ya kuanza kazi hiyo na pindi wakimaliza nitamalizia pesa iliyosalia "
Hata hivyo mbunge Mwamoto aliwataka wananchi kuendelea kuchangia shughuli za kimaendeleo hasa elimu na kuwa serikali ya Rais Dr John Magufuli imefuta michango na ada kwa elimu ya msingi na sekondari na sio kwamba imefuta michango ya ujenzi wa nyumba za walimu ama shule .
Hivyo aliwataka wananchi kuendelea jitihada zao za kushiriki kuchangia maendeleo ya elimu kwa maana ya ujenzi wakati serikali imechukua jukumu la kuwalipia watoto hao ada na chakula kwa shule za sekondari za bweni ambazo zipo chini ya serikali.
Alisema kuwa yeye kama mbunge wao kamwe hata waacha yatima katika shughuli yoyote ya kimaendeleo atahakikisha anashirikiana na wananchi hao kikamilifu katika kuitekeleza .
Afisa mtendaji wa kata ya Ilulu Bw Chusi Ashrafu akimpongeza mbunge Mwamoto kwa kuunga mkono nguvu za wananchi hao alisema kuwa hadi sasa mwitikio wa wananchi katika shughuli za kimaendeleo ikiwemo ya umaliziaji wa madarasa hayo ni nzuri .
Alisema hadi sasa wananchi wa vitongiji vyote vitatu wameonyesha ushirikiano mzuri zaidi kwa kila kitongoji kuchangia kiasi cha Tsh 200,000 na wana jumla ya Tsh 600,000 kati ya Tsh milioni 1 ambayo wananchi walipaswa kuchangia wakati mbunge akiahidi kuchangia Tsh milioni 1 na kwa sasa mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo pia ameahidi kumuunga mkono Mbunge Mwamoto kwa kuchangia Tsh 200,000 hivyo wanamatumaini kasi ya ujenzi huo hadi sasa imefikia pazuri zaidi.
No comments:
Post a Comment