Rais Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu (pichani).
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa pamoja na kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi pia Mkurugenzi wa Tehama, Joseph Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima nao wamesimamishwa kazi.
Mwaimu |
Balozi Sefue |

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari, Ikulu Dar es Salaam leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu, ili kupisha vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi. (Picha na Francis Dande)
Taarifa zilizomfikia Rais zinaonesha kuwa NIDA hadi sasa imetumia Shs. Bilioni 179.6 kiasi hiki ni kikubwa na Rais angependa ufanyike uchunguzi na ukaguzi wa jinsi fedha hizi zilivyotumika, maana Rais amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na kasi ndogo ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.
Hivyo, Rais ameelekeza Mamlaka ya Udhibiti na Manunuzi ya Umma (PPRA) wafanye ukaguzi maalum wa manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA.
Rais Pia ameelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanye ukaguzi maalum wa hesabu za NIDA, ikiwemo ukaguzi wa 'Value for Money' baada ya kuthibitisha idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa hadi sasa.
Rais ameelekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ifanye uchunguzi kujiridhisha kama kulikuwa na vitendo vya rushwa au la.

MIAKA MITANO SIJAPATA KITAMBULISHO, NILIJIANDIKISHA KIMARA BONYOKWA FOMU ZIKAPOTEA, NIKAAMBIWA NIENDE MBEZI NAKO FOMU ZIKAPOTEA, NIKAAMBIWA NIENDE NIDA KINONDONI MIEZA 5 sasa NAAMBIWA KIMTAMBULISHO KIMETOKA HAKIJULIKANI KILIPO NJOO BAADA YA MWEZI HAWA LAZIMA WANG'OKE SIO KUWAONEA HURUMA SI WAO NA WAKE WADOGO PIA
ReplyDeleteWASOMI WA IT WAKO WENGI SANA HAWANA KAZI WAAJIRIWE