NA GLORY CHACKY
MTOTO wa mwaka mmoja na nusu amebakwa na kulawitiwa na baba yake wa kufikia
John Donald (35) mkazi wa Kiyangu, Manispaa ya Mikindani mkoani Mtwara.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini Dar es salaam na msemaji wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Erasto Ching’oro, inakemea vikali
kitendo hicho.
Taarifa
hiyo inasema kubakwa
na kulawitiwa ni ukatili wa hali ya juu dhidi ya mtoto maana husababisha maumivu
makali ikiwa ni pamoja na kumdhuru mtoto kimwili, kisaikolojia, kijamii na
kihisia.
Aidha, vitendo hivi, vinaacha kovu la kudumu
kimwilini, kiakili, kimaadili, kijamii, ulemavu, maumivu, na wakati mwingine
husababisha kifo, jambo ambalo linahitaji ulinzi thabiti katika kuhakikisha
watoto wanaishi mazingira salama na rafiki.
Kitendo hicho ni ukiukwaji mkubwa wa haki za mtoto
ambao huchangia kurudisha nyuma ustawi na maendeleo ya Mtoto na ni kinyume cha
Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009.
Pia taarifa hiyo inasema mtuhumiwa amekamatwa na
kufikishwa mahakamani ili hatua za kusheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Wizara inamwelekeza Afisa Ustawi wa Jamii na Afisa
Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Mtwara kuwasiliana na wadau wengine katika ngazi
zote kuhakikisha mama na mtoto wanapata huduma ya afya na ushauri na kufuatilia mwenendo wa shauri hilo.
No comments:
Post a Comment