NA KENNETH NGELESI, MBEYA
KATIKA harakati za Serikali kubana matumizi imetenga Hekta tano za ardhi Wilayani Kibaha Mkoani Pwani kwa ajili ya ujenzi wa ghala ya ambalo litakuwa likitumiwa na Bohari ya dawa nchini (MSD) kwa ajili kuifadhiwa dawa pamoja na vifaa tiba.
Taarifa hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Afya,Maendeo ya Jamii,Jinsia watoto na wazee Ummy Mwalimu wakati akizindua Duka na Dawa lilipo chini ya Bohari hiyo eneo Forest ya zamani pamoja na Ghala jipya la kuifadhia dawa lilipo Iwambi jiji Mbeya.
Mwalimu alisema kuwa ardhi hiyo imetolewa na Rais John Pombe Magufuli ambapo likisha kamilika litakuwa limepusha upotevu wa fedha shilingi biloni 4 ambazo zimekuwa zitimika kila mwaka kwa ajili ya kulipia kodi ya maghala ya kukodi.
Aidha katika hatua nyingine Mwalimu alisema kuwa Serikali inandaa utaratibu utakao wawaweza wanachama wa mifuko ya Afya ya Jamii. NHIF pamoja CHI kupata dawa kupitia maduka ya Msd badala ya sasa ambapo wanachama hao wamekuwa wakinunua dawa kwenye maduka ya watu binafsi.
Alisema kuwa kwa kufanya hivyo kutaweza kuhamasishi wananchi wengi kujinga na mifuko tofauti na sasa ambapo kwa sasa hamasa ya kujiunga na mifuko hiyo ikiwa chini huku akieleza kuwa sasbabu ni kutokna na changamoto ya dawa kutoa patikana na kwenye Zahanati,Vituo vyua Afya na Hospitali mbalimbali.
‘Ni kweli kumekuwa na changamoto ya wananchi kutoa jiunga na mifuko hiyo lakini changamoto kubwa ni pale anapo fika kwenye Zahanati zetu anakuta dawa hazipo lakini kwa kuliona hili tunaanda utaratibu namna watakovyo pata dawa moja moja kwenye maduka ya msd na nina imani hili litaongeza kasi wananchi kujiunga na mifuko hii’ alisema Mwalimu.
Alisema kuwa lengo la Serikali la kufungua maduka katika Hospitali ni kuwaewezesha wananchi wote kuweza kupata huduma ya dawa pamoja na vifaa tiba kwa bei ndogo na kwa uraisi zaidi ambayo kila mwanchi anaweza kuimudu.
Aidha alisema kuwa pamoja na juhudi hizo za Serikali za kuhakikisha wananchi wanapata dawa kwa uraisi lakini kubwa ni changamoto watumishi wa afya wasio waaminifu ambao wamekuwa wakiiba dawa na kwenda kuziuza kwenye maduka maduka binafsi.
Kutokana na hilo Waziri Mwalimu amewagiza wakuu wote wa Mikoa na Wilaya pamoja na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa Serikali ikiwa ni pamoja na kuwa fichua watumishi wote wanao jihusisha na vitendo vya wizi dawa.
Mwalimu ambaye yupo Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi alisema kuwa Serikali imedhamiria kuboresha huduma ya afya na ndiyo maana ikaiamuru bohari ya dawa kuwa na maduka katika Hospitali mbalimbali, hivyo haitakuwa tayari kuwavumia watumishi wote ambayo wanahujumu juhudi za Serikali.
Awali akisoma taarifa ya Bohari ya dawa nchini Laurean Bwanakunu Mkurugenzi wa Bohari ya dawa alisema kufungua kwa duka hilo na kutelekeza agizo la Rais Magufuli ambapo mpaka sasa msd imeshafungua maduka matano nchi nzima.
Alisema kuwa duka la Mbeya ni miongoni mwa maduka matano yaliofunguliwa kote ambayo ni Geita,Arusha Hospital ya Mount Meru,Hospital ya Taifa ya Muhimbili na Mwanza.
No comments:
Post a Comment