TIMU ya soka ya Uchukuzi SC
imeng’ara kwa kuifunga Ukaguzi mabao 3-1 katika mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea
kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Uchukuzi SC ambayo chini ya benchi
la ufundi mahiri linaloongozwa na Kenneth Mwaisabula ‘Mzazi’ ambaye ni Mkuu wa
benchi hilo, huku Elutery Muholeli
ni kocha na Robert Damian ni meneja wa timu hiyo, waliwapeleka puta wapinzani
wao na kuandika bao la kwanza lililofungwa kwa kichwa na Kado Nyoni, baada ya
kuwahi mpira wa kona safi iliyochongwa na Omar Said ‘Chidi’ katika dakika ya
34.
Hatahivyo,
Ukaguzi walisawazisha katika dakika ya 50 kupitia kwa Ben Chezue aliyepiga
mpira wa adhabu ndogo uliokwenda moja kwa moja golini.
Chezue aliingia dakika
49 kuchukua nafasi ya Deo Masanja
aliyekuwa ameumia, Uchukuzi
SC iliongeza bao katika dakika ya 72 lililofungwa Issac Ibrahim aliyeachia
shuti kali, lililomshinda kipa wa Ukaguzi, Shomari Dumba.
Nahodha
wa Uchukuzi SC, Francis Charles alipigilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao la
tatu katika dakika ya 90 kwa njia ya penati baada ya Bilal Mleli kushika mpira
katika eneo la hatari.
Uchukuzi
SC iliyokuwa ikicheza kwa kuonana, awali timu Uchukuzi SC ilikosa magoli kibao
ya wazi, baada ya wachezaji wake Abubakar Mwamonchi katika dakika ya 25 kupiga
mpira uliopita pembeni kidogo ya goli, huku Francis alishindwa kuunganisha
krosi ya Masoud Juma katika dakika ya 30, tena Francis aliyeisumbua ngome ya
Ukaguzi katika dakika ya 58 alipaisha mpira akiwa karibu na kipa.
Akizungumza
mara baada ya mechi, kocha Muholeli alisema Ukaguzi ni moja ya timu ngumu,
lakini aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kutoka na ushindi
mnono, ambao umesaidia kusafisha njia.
“Hapa
tumekuja kushindana na kila mechi kwetu tunaiita ni fainali, hivyo timu zote zilizokuja
hapa ni nzuri, ila tunataka tushinde mechi zote ili tujiweke pazuri kushinda na
kutwaa kombe hili, kwani tumeshafika fainali mara nne,” alisema Muholeli.
Naye
Mwenyekiti wa Uchukuzi SC, Mohamed Ally alisema wamekuja Dodoma kuchukua
ubingwa na anauhakika wa timu yake itafanya vyema kutokana na nidhamu ya
mazoezi wanayofanya kila siku.
Kikosi
cha ushindi cha Uchukuzi SC ni: Barton Willy, Ally Poloto, Omar Said ‘Chidi’,
Godwin Ponda, Kado Nyoni, Fidelis Kyangu, Seleman Kaitaba/Issac Ibrahim (63),
Francis Charles, Ramadhani Madebe, Abubakar Mwamachi/Omar Kitambo (35), na
Masoud Juma/Michael Bernad (46).
Kikosi cha Uchukuzi SC kabla ya mechi na Ukaguzi.
Mchezaji wa Uchukuzi SC, Godwin Ponda (namba 6 mgongoni) akiwania mpira kutoka kwa wachezaji wa Ukaguzi.
Mkuu wa benchi la ufundi la timu ya soka ya Uchukuzi SC, Kenneth Mwaisabula (kulia) akiongea na mmoja wa wachezaji wa timu ya Ukaguzi, mara baada ya mchezo wao kumalizika. Uchukuzi walishinda kwa magoli 3-1.
Wachezaji wa timu mbalimbali za Uchukuzi SC wakishangia mara baada ya mchezo wa soka dhidi ya Ukaguzi kumalizika. Uchukuzi iliibuka mshindi kwa magoli 3-1.
Masoud Juma (kushoto) wa timu ya soka ya Uchukuzi SC akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Mkoa wa Dodoma (DOREFA), Nassoro Kipenzi (kulia).
Mchezaji wa timu ya Uchukuzi SC, Omar Said `Chidi’ (mwenye namba 8 mgongoni) akiwania mpira na Ukaguzi.
Mchezaji wa timu ya Uchukuzi SC, Abubakar Mwamachi (mwenye namba 22 mgongoni) akifunga kwa kichwa bao la kwanza. Uchukuzi iliishinda Ukaguzi kwa magoli 3-1.
Kocha wa timu ya Uchukuzi SC, Elutery Muholeli (wa pili kulia) akiwaelekeza wachezaji wake, wakati wa medhi yao dhidi ya Ukaguzi.
No comments:
Post a Comment