May 26, 2016

CAF YAMTEUA MICHAEL WAMBURA

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua Michael Richard Wambura kuwa Kamishna wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Rwanda na Msumbiji unaotarajiwa kufanyika jijini Kigali, Juni 3, 2016.

Wambura ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), atakuwa Balozi mzuri katika mchezo huo unaokutanisha timu ambazo nchi imepana nazo. Msumbiji iko Kusini mwa Tanzania wakati Rwanda iko Magharibi mwa Tanzania.

Taarifa hii haina link ya maelezo zaidi

TAIFA STARS KWENDA KENYA KESHO

Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania – Taifa Stars, chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco kinatarajiwa kuondoka kesho saa 12.00 alfajiri kwenda Nairobi, Kenya kucheza na Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Mchezo huo ni maandalizi ya kujiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017) wakati Kenya pia itakuwa na mchezo dhidi ya Congo.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

SERENGETI BOYS

Karibuni waandishi habari na wadau wengine kuilaki timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ inayotarajiwa kutua leo Mei 26, 2016 saa 1.15 jioni baada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano maalumu ya kimataifa iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIF Youth Cup 2016 U-16).

Serengeti Boys haikuwahi kupoteza mchezo hata mmoja katika michuano hiyo baada ya kutoka sare mechi tatu na kushinda mmoja kabla ya kuingia hatua ya kucheza mshindi wa tatu ambako ilishinda mabao 3-0 jana dhidi ya Malaysia.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

 
AZAM NA TFF

Kesho Ijumaa MEI 27, 2016 saa 5.00 asubuhi kutakuwa hafla fupi na maendeleo ya soka nchini kati ya uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kampuni ya Azam itakayofanyika kwenye ofisi ya Azam zilizoko Tazara kwenye makutano ya barabara za Nyerere na Mandela, Dar es Salaam. Waandishi wote wa habari mnaalikwa kwenye hafla hiyo. Karibuni sana.

No comments:

Post a Comment

Pages