May 20, 2016

JIJI LA ARUSHA LAPOKEA VIFAA VYA MAMILIONI KUTOKA UMOJA WA MATAIFA

Mkuu wa Utawala wa iliyokua Mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda (ICTR) Sarah Kilemi(wa tatu kulia) akiwakabidhi funguo za gari aina ya Mitsubishi Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro na Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji hilo,Juma Idd.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Arusha,Juma Idd(kulia) akiweka saini makubaliano kwaajili ya kukabidhiwa gari aina ya Mitsubishi na mashine ya kisasa ya kuzima moto akishuhudiwa na viongozi wa jiji na Mkuu wa Utawala wa iliyokua mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda(ICTR)Sarah Kilemi,kulia kwake.


Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro akipanda kwenye gari hilo wakati wa makabidhiano hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Arusha,Juma Idd(kulia) akizungumza na mmoja wa Askari wa Umoja wa Mataifa(UN)wanaoimarisha ulinzi eneo hilo.


Afisa Uhusiano wa Jiji la Arusha,Nteghenjwa Hoseah akifurahia gari hilo.

Mashine ya kisasa ya kuzimamoto inayotumia nguvu za Umeme na Petroli yenye uwezo wa kusukuma maji kwenye majengo yenye ghorofa zaidi 100.

Sehemu ya vifaa hivyo vya aina yake ambavyo vitasaidia wakati wa majanga yanapotokea.

No comments:

Post a Comment

Pages