May 12, 2016

MAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA,RAJABU AKIZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA CCM MKOA WA PWANI

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Rajab Luhwavi akizungumza na wafanyakazi wa CCM kutoka wilaya zote za mkoa wa Pwani, katika kikao chake na wafanyakazi hao kilichofanyika wilayani Kibaha mkoa wa Pwani. (Picha na Bashir Nkoromo).
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara, Rajab Luhwavi akivishwa Skafu na Kijana wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Omari Salum, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, Wilayani Kibaha mkoani humo leo.  Katikati ni Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga na kulia ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Kibaha,  David Malecela.


Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwai akisalimia baadhi ya viongozi baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, kuzungmza na wafanyakazi wa CCM mkoa huo, leo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Rajab Luhwavi akisaibi kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, iliyopo wilayani Kibaha leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Pwani, Joyce Masunga.
Watumishi wa CCM katika mkoa wa Pwani, wakimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu Luhwavi alipokaribia kuingia katika ukumbi kufanya kikao na wafanyakazi hao katika Ofisi ya CCM ya mkoa, iliyopo Kibaha.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu Luhwavi akiwasili ukumbini katika Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani iliyopo Kibaha,  tayari kuzungumza na wafanyakazi wa CCM kutoka wilaya zote za mkoa wa Pwani, leo.

No comments:

Post a Comment

Pages