May 03, 2016

TANESCO MBEYA YAIDAI SERIKALI BILIONI 7.3, MGODI WA KIWILA BILIONI1.2

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

SHIRIKA la umeme ‘TANESCO’ mkoani Mbeya limemuomba Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla kutumia nafasi yake kuzihamasisha taasisi za Serikali kulipa deni la shiriki bilioni 7.3 ili shirika hilo liweze kutekeleza miradi  iliyo kwama kutoka na ukosefu wa fedha.


Akisoma taararifa ya shirika hilo Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mbeya Mhandisi Francis Maza, mbele ya Mkuu wa Mkoa alisema asilimia kubwa ya shirika hilo linajiendesha hivyo ucheleweshwaji wa deni hilo unakwamisha juhudi za shirika hilo kakamilisha miradi ya mipya hasa vijijini kwa wakati.

Alisema hadi Machi 31 mwaka huu  taasisi za Serikali ndiyo wadaiwa sugu wa shirika hilo huku mgodi wa Kiwila ‘Kiwila Coal Mine “ukidaiwa shilindi bilioni 1.2 ukifatiwa na Jeshi la polisi linalo daiwa shilingi milioni 442.9.

Aidha katika hatua nyingine Meneja huyo alibainisha baadhi ya taasisi zingine zinadaiwa na shirika hilo kwa Mkoa wa Mbeya kuwa ni Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) Milioni 100.7, JKT, milioni 18, Jeshi la Magereza sh. Milioni 372, Hospitali za serikali sh. Milioni 63.1, Taasisi na Idara zingine za serikali sh. Milioni 348, na wateja wa kawaida
sh. Bilioni 4.8.

Akijibu  taarifa hiyo alisema kuwa yupo tayari kulifanyia kazi suala na kwamba atakutana na mawziri wenye dhamana pamoja na wakuu wa iadara hizo kuangalia namna ya kulopa fedha na kwamba ikibidi  ziingizwe moja kwa moja kwenye akaount ya shirika  badala ya kupitia kwenye taasisi zenyewe ambapo alidai kuwa wakati mwingine hubadilisha matumizi kinyume na utaratibu na maagizo ya Serikali.


‘ Nisema wazi nimelipokea na pia nimekubali nitawasiliana na mawaziri wa taasisi husika kuhusu kulipa madeni yao haraka, lakini pia nitumie fursa hii kuzisii taasisi husika kulipa madeni hayo haraka kwani fedha hizo ni nyingi mimi kama mkuu wa mkoa nitazikumbusha hizi taasisi pamoja na waziri husika ili kulipa hizo fedha kuwa kuwa shirika linatakiwa kujiendesha’ alisema Makalla.

Katoa hatau nyingine  Makalla aliwataka watumishi wa shirika hilo  kuacha urafiki na watu wanajiunganishia umeme kinyume na  utaratibu maarufu kama ‘vishoka’  kwani wamekuwa wakiwachanganya wananchi.

Alisema kuwa vishoka wamekuwa wakichukua fedha nyingi kutoka kwa wananchi kwa lengo la kuwaunganishia umeme jambo linalopelekea wananchi kuwa na manung’uniko kwa tanesco na seikali kwa ujumla.

Makala alisema vitendo hivyo haviwezi kuisha ikiwa wafanyakazi wa Tanesco wataendeleza urafiki na vishoka kwa kupewa hongo na rushwa kwab lengo la kuunganisha umeme.

“Vishoka wanakula na nyinyi watumishi wa tanesco, kutokana na kujenga urafiki na nyinyi na wananguvu ya pesa kuliko nyie,wanawaibia wananchi fedha nyingi kwa kisingizio cha kuwaunganishia umeme, sasa nasema acheni urafiki na hao watu wanasababisha wananchi kulichukia shirika.”alisema

No comments:

Post a Comment

Pages