May 21, 2016

TRA YAWAPA ELIMU YA MLIPAKODI WAFANYABIASHARA RAIA WA CHINA WAISHIO NCHINI TANZANIA

1
Meneja wa Elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA Bi. Diana Masalla akitoa elimu ya mlipa kodi na sheria za kodi kwa wafanyabiashara raia wa China wanaoishi hapa nchini na kufanya biashara katika semina ya mlipa kodi iliyofanyika leo kwenye mgahawa wa Tang Ren Chinese jijini Dar es salaam, ambapo kabla semina hiyo imefunguliwa na Bw. Sun Chengfeng Mwakilishi wa masuala ya Kiuchumi na Kibiashara kutoka serikali ya Watu wa China nchini Tanzania, Semina hiyo inalenga kuwapa wafanyabiashara hao elimu na uelewa wa masuala mbalimbali ya kisheria katika kodi na umuhimu wa kulipa kodi.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE)
3
Baadhi ya wafanyabiashara raia wa China wanaoishi nchini Tanzania na kufanya biashara wakiwa katika semina ya mlipa kodi iliyofanyika leo kwenye mgahawa wa Tang Ren Chinese jijini Dar es salaam
4
Bw. Sun Chengfeng Mwakilishi wa masuala ya Kiuchumi na Kibashara kutoka Serikali ya Watu wa China nchini Tanzania akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina hiyo iliyofanyika kwenye mgahawa wa Tang Ren Chinese jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages