HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2016

MALINZI APONGEZA UONGOZI MPYA BUNGE FC

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, amepongeza uongozi wa timu ya Bunge FC uliochaguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Dodoma.

Viongozi waliochaguliwa ni Mwenyekiti Mhe. William Ngeleja (CCM); Makamu Mwenyekiti, Mhe. Esther Matiko; Meneja wa Klabu, John Kadutu pamoja Wajumbe ambao ni Mhe. Neema Mgaya, Mhe. Faida Bakari, Mhe. CosatoChumi, Mhe. Anna Lupembe na Mhe. Grace Kihwelu.

Rais Malinzi amewatakia kila la kheri Bunge Sports Club na kuwaahidi ushirikiano kutoka TFF katika kuendeleza klabu yao na michezo kwa ujumla.


No comments:

Post a Comment

Pages