July 20, 2016

SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII NSSF LATAO HUDUMA YA UPIMAJI AFYA BURE KATIKA ENEO LA TPC MOSHI



Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF Limefanya zoezi la upimaji afya kwa wafanyakazi  wa kiwanda cha sukari TPC na Wananchi wa eneo hilo.

 Kwa miaka kadhaa imekuwa ikiendesha zoezi hili katika maeneo mbalimbali hapa nchini, Lengo la zoezi hili ni kuwapa Fursa Wanachama na wasio Wanachama wa NSSF kuweze kujua mwenendo wa Afya zao bila kutumia gharama yeyote na kuisaidia serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini. 

Zoezi Hilo lilienda sambamba na zoezi la Uchangiaji wa damu salama kutoka kwa Wananchi wa eneo la TPC.
Mpango huu unaenda sambamba na mpango wa matibabu bure kwa wanachama kupitia SHIB ambapo  kwa TPC, Hospitali ya TPC iliweza kupata usajili mwaka 2012 wa kutoa matibabu bure kwa Wanachama wa NSSF. 

Hadi sasa TPC ina jumla ya wachama 1121 wanaopata matibabu  kupitia NSSF, wategemezi 2764 wanaofadikia na mpango wa matibabu bure kutoka NSSF, Mpaka sasa NSSF imekwisha lipa takribani  shilingi 720 mil kuanzia mwaka 2012  kama gharama za kutoa matibabu  kwa wanachama.

Mbali na hayo Fedha zilizokuwa zikilipwa na NSSF kwa ajili ya matibabu hayo zimesaidia kuboresha huduma katika  hospitali ya  TPC na kuchangia ujenzi wa chumba cha upasuaji na vifaa  tiba kwenye chumba hicho, kununua mashine ya Ultra saound. Uboreshaji huu wa huduma umewezesha  kuboresha huduma za afya na kusogeza huduma za afya Karibu na Wananchi.
Mmoja wa wanachama wa Shirika la taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF), akipatiwa huduma ya Vipimo kutoka kwa Daktari wa NSSF, Aisha Abeid  katika zoezi la upimaji afya kwa hiari lililofanyika katika eneo la kiwanda cha TPC Mjini Moshi, juzi. (Na Mpigapicha Wetu)
Mwanachama wa NSSF akipatiwa huduma ya Vipimo kutoka kwa Daktari wa NSSF Mrs Mariam Msuri katika zoezi la upimaji afya kwa hiari lililofanyika katika eneo la kiwanda cha TPC Mjini Moshi

Mwananchi wa Eneo la TPC akichangia damu wakati wa zoezi la upimaji afya kwa hiari lililofanyika katika eneo la kiwanda cha TPC Mjini Moshi

Wafanyakazi na Wananchi wa eneo Kiwanda cha TPC wakipata Maelezo kuhusu uanachama wa HIARI kutoa kwa Mkuu wa Ofisi ndogo ya NSSF TPC, Kambaga wakati wa zoezi la upimaji afya kwa hiari lililofanyika katika eneo la kiwanda cha TPC Mjini Moshi.
Meneja Kiongozi wa NSSF wa mkoa wa Kilimanjaro, Delphina Masika na Meneja wa Mafao ya Matibabu Dk. Aly Mtulia wakipata Maelezo kuhusu upimaji Afya kutoka kwa Mganga wa Hospitali ya TPC.

Mwanachama wa NSSF akipima  uzito na Urefu katika zoezi la upimaji afya kwa hiari lililofanyika katika eneo la kiwanda cha TPC Mjini Moshi.

No comments:

Post a Comment

Pages