Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF Limefanya zoezi la
upimaji afya kwa wafanyakazi wa kiwanda cha sukari TPC na Wananchi wa
eneo hilo.
Kwa miaka kadhaa imekuwa ikiendesha zoezi hili katika
maeneo mbalimbali hapa nchini, Lengo la zoezi hili ni kuwapa Fursa Wanachama na
wasio Wanachama wa NSSF kuweze kujua mwenendo wa Afya zao bila kutumia gharama
yeyote na kuisaidia serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini.
Zoezi Hilo lilienda sambamba na zoezi la Uchangiaji wa damu
salama kutoka kwa Wananchi wa eneo la TPC.
Mpango huu unaenda sambamba na mpango wa matibabu bure kwa
wanachama kupitia SHIB ambapo kwa TPC, Hospitali ya TPC iliweza kupata
usajili mwaka 2012 wa kutoa matibabu bure kwa Wanachama wa NSSF.
Hadi sasa TPC
ina jumla ya wachama 1121 wanaopata matibabu kupitia NSSF, wategemezi
2764 wanaofadikia na mpango wa matibabu bure kutoka NSSF, Mpaka sasa NSSF
imekwisha lipa takribani shilingi 720 mil kuanzia mwaka 2012 kama
gharama za kutoa matibabu kwa wanachama.
Mbali na hayo Fedha zilizokuwa zikilipwa na NSSF kwa ajili
ya matibabu hayo zimesaidia kuboresha huduma katika hospitali ya
TPC na kuchangia ujenzi wa chumba cha upasuaji na vifaa tiba kwenye
chumba hicho, kununua mashine ya Ultra saound. Uboreshaji huu wa huduma
umewezesha kuboresha huduma za afya na kusogeza huduma za afya Karibu na
Wananchi.
Mmoja wa wanachama wa Shirika la taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF),
akipatiwa huduma ya Vipimo kutoka kwa Daktari wa NSSF, Aisha Abeid katika zoezi la upimaji afya kwa hiari
lililofanyika katika eneo la kiwanda cha TPC Mjini Moshi, juzi. (Na Mpigapicha
Wetu)
Mwanachama wa NSSF akipatiwa
huduma ya Vipimo kutoka kwa Daktari wa NSSF Mrs Mariam Msuri katika zoezi la
upimaji afya kwa hiari lililofanyika katika eneo la kiwanda cha TPC Mjini Moshi
Mwananchi wa Eneo la TPC akichangia damu wakati wa zoezi la upimaji afya kwa hiari lililofanyika katika eneo la kiwanda cha TPC Mjini Moshi
Wafanyakazi na Wananchi wa eneo Kiwanda cha TPC wakipata Maelezo kuhusu uanachama wa HIARI kutoa kwa Mkuu wa Ofisi ndogo ya NSSF TPC, Kambaga wakati wa zoezi la upimaji afya kwa hiari lililofanyika katika eneo la kiwanda cha TPC Mjini Moshi.
Meneja Kiongozi wa NSSF wa
mkoa wa Kilimanjaro, Delphina Masika na Meneja wa Mafao ya Matibabu Dk. Aly
Mtulia wakipata Maelezo kuhusu upimaji Afya kutoka kwa Mganga wa Hospitali ya
TPC.


No comments:
Post a Comment