Nyota
wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti
Boys wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O.R. Tambo jijini Johannesburg,
Afrika Kusini wakitokea Antananarivo, Madagascar walikoweka kambi kujiandaa na
mchezo dhidi ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki
fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye huo hapo mwakani. Serengeti Boys
itakipiga na Afrika Kusini Jumamosi kwenye Uwanja wa Dobsonville, Johannesburg,
Afrika Kusini. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)
Baadhi
ya Viongozi wa wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka
17 – Serengeti Boys wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O.R. Tambo jijini
Johannesburg, Afrika Kusini wakitokea Antananarivo, Madagascar. Kutoka kushoto
ni Ayoub Nyenzi, Pelegrinus Rutayuga na Mshauri wa Ufundi, Kim Poulsen. Serengeti
Boys itakipiga na Afrika Kusini Jumamosi kwenye Uwanja wa Dobsonville,
Johannesburg, Afrika Kusini. (Picha na Alfred Lucas wa TFF).
No comments:
Post a Comment