HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 17, 2016

JOGGING SIO UHUNI,KUNA WATU WALITAKA KUPENYEZA MAMBO YAO NA KUTAKA KUICHAFUA JOGGING- DC ILALA

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema (pili kulia) akiwa sambamba na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo (tatu kushoto) wakishiriki mazoezi ya pamoja ya kikundi cha klabu ya Mazoezi cha New Life Jogging,na vikundi vingine mbalimbali vya mazoezi , mapema leo asubuhi katika viwanja vya Kimanga,Tabata Mawenzi,jijini Dar,ambapo Mkuu wa Wilaya alialikwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla fupi ya kikundi cha New Life Jogging kilipokuwa kinatimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.PICHA NA MICHUZI JR-MMG.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema akikabidhiwa Risala na Mwenyekiti wa kikundi cha Newa Life Jogging,Baraka Urio akiwa ameambatana na wanachama wa kikundi hicho,mara baada ya kuisoma na kuelezea changamoto na fursa mbalimbali zilizopo ndani ya kikundi hicho.Kikundi hicho chenye makazi yake Tabata Mawenzi leo kimetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema akizungumza mbele ya vikundi mbalimbali vya mazoezi (havipo pichani),vilivyoshiriki kwenye hafla hiyo fupi ya kutimizwa mwaka mmoja wa kikundi cha New Life Jogging.Mh.Mjema aliwataka viongozi wa vikundi hivyo kuelezea changamoto zao walizo nazo ikiwemo na fursa zilizopo ili serikali kupitia Ofisi yake ziweze kufanyiwa kazi kwa wakati.Mh Mjema alisema kuwa Jogging sio uhuni,isipokuwa kuna watu walitaka kupenyeza mambo yao katika Jogging.

"Lakini wale waliotaka kuyapenyeza hayo,waliotaka kuingiza uhalifu,waliotaka kupenyeza madawa ya kulevya ,waliotaka kuingiza siasa,waliotaka kuingiza Panya rodi washindwe na walegee,hatutaki Jogging zetu zichafuke,tunataka Jogging zitumike kuona fursa zilizopo",alisema Mh Mjema.
Katibu Tawala wilaya ya Ilala, Ndugu Edward Mpogolo akiwasalimia na kuwatia moyo vikundi hivyo vya Jogging,ambaye pia aliwaeleza kuwa wakati wa kujituna na kufanya kazi ni sasa,hivyo amewaomba viongozi wa vikundi hivyo kukutana nao ili kuhakikisha fursa na changamoto walizozieleza katika risala yao zinafanyiwa kazi kwa wakati.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema akikabidhiwa jezi na Mwenyekiti wa kikundi cha New Life Jogging,Baraka Urio,pichani kati ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala,Ndugu Edward Mpogolo na wadau wengine wakishuhudia tukio hilo.
Mgeni rasmi,Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Sophia Mjema na viongozi wengine waandamizi kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya wakiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha New Life Jogging,ambacho leo kinasherehekea kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.
Vikundi mbalimbali vilishiriki kwenye mazoezi hayo ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Pages