October 21, 2016

PLATINUM CREDIT TANZANIA YACHANGIA MAAFA YA KAGERA



Afisa masoko Platinum Credit Tanzania, Gideon Lufunyo (kushoto) akikabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji ambayo ni sawa na tani 15 kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu ikiwa ni msaada wa taasisi hiyo kwa waathirika wa tetemeko la Ardhi mkoani humo.
Kampuni ya Platnum Credit Tanzania Leo imekabidhi msaada wa mifuko 300 ya sumenti kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni mkoani humo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo leo, Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo,Gideon Lufunyo alisema  tetemeko hilo limeleta madhara makubwa ambayo yamewagusa na kuamua kusaidia serikali katika kurejesha miundombinu yake hasa katika mshule katika hali nzuri ili masomo yaendelee na watoto wapate elimu.

No comments:

Post a Comment

Pages