October 21, 2016

RAIS DK. JOHN MAGUFULI AKINDUA MRADI WA UJENZI WA HOSTELI ZA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

 Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Jouce Ndalichako akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Humphrey Polepole muda mfupi kabla ya Rais Dk. John Magufuli hajazindua mradi wa ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako akizungumza katika hafla hiyo.

 Rais Dk. John Magufuli akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Muonekano wa majengo ya hosteli hizo.
Wasanii wa kikundi cha JKT wakitumbuiza katika hafla hiyo.
 Rais Dk. John Magufuli akipata maelezo ya ujenzi wa hosteli hizo.
Rais John Magufuli akisalimiana na Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso), Erasmo Leon mara baada ya kuzindua mradi wa Ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa Chuo hicho jijini Dar es Salaam. 
 Rais John Magufuli akipiga tumba wakati benki ya Msongo Ngoma ilipokuwa ikitumbuiza katika hafla hiyo.
Rais John Magufuli akizindua mradi wa ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kampasi ya Mwalimu Nyerere, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Rais John Magufuli (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kampasi ya Mwalimu Nyerere, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

Pages