October 28, 2016

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA KUFANYIKA ZANZIBAR


Na Mpiga Picha Wetu

UBALOZI wa Ujerumani umetangaza kudhamini tamasha la mziki kwa Afrika mashariki liitwalo Sauti za busara litakalo fanyika Zanzibar kwanzia februari 9 hadi 12 mwaka kesho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa , balozi Ego Kochanke na mwenyekiti wa  tamasha hilo Mohammed Said wamesaini mkataba wa makubaliano wa 5,000.

Toka mwaka 2004 sauti za busara zimekuwa zikisherekewa afrika mashariki na kuwakutanisha wanamuziki wa wilaya, mikoa na hata kimataifa.

Mwakani Pat Thomas na Area Band kutoka Ujerumani watashiriki na kutoa burudani katika siku zote nne za tamasha hilo.

Sauti za busara limetoholewa kwenye neon la kingereza ‘Sound of Wisdom’ na kwamba tamasha hilo limekuwa likisapoti sana mziki wa Afrika hasa mziki wa asili ambao ni wakipee na kolabo kutoka kwa wasanii mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages