Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa
Kiuchumi na Kijamii, (ESRF), Dkt. Tausi Mbaga Kida, (kulia), akizungumza kwenye Warsha ya majadiliano ya wadau kuhusu nafasi ya sekta binafsi katika kutekeleza mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano (FYDPII), kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoawa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka
Naibu Katibu Mkuu Tume ya Mipango, kutoka Wiraza ya Fedha na Mipango, Dkt. Maduka Paul Kessy(kushoto0, akizungumza kwenye warsha hiyo. |
Mkurugenzi wa Huaduma kwa Wanachama, Taasisi ya Sekta Binafsi, (TPSF), Bw. Louis Accaro, akitoa mada yake juu ya sekta za kipaumbele ambazo zinapaswa kujadiliwa ili kufanyiwa kazi, sekta hizo ni kutoka zao la Pamba na kuwa nguo, kutoka ngozi na kuwa mazao yatokanayo na ngozi, na pia viwanda vya madawa
Baadhi yawashiriki wa warsha wakifuatilia mjadala
Baadhi ya washiriki.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka, akizungumza wakati wa warsha hiyo. |
NA
K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
WADAU kutoka kada mbalimbali wamekutana kujadiliana
jinsi sekta binafsi itakavyoshiriki katika utekelezaji thabiti wa mpango wa
pili wa miaka mitano wa maendeleo ya Tanzania kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF
jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii, (ESRF), Dkt. Tausi Mbaga Kida,
amesema sekta binafsi inao umuhimu mkubwa katika kushiriki kuandaaa na kujadili
mipango mbalimbali ya maendeleo.
Dkt. Kida aliyasema
hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Warsha ya majadiliano kuhusu nafasi ya
sekta binafsi katika kutekeleza mpango wa pili wa miaka mitano wa maendeleo ya
Tanzania, (FYDP II) iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar
es Salaam.
Warsha hiyo iliyoandaliwa
kwa pamoja na ESRF, Serikali kupitia Tume ya Mipango na Mpango wa Kusaidia
Mabadiliko ya Kiuchumi, (SET), iliwakutanisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja
na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, (TPSF), CEO roundtable, Suma JKT, Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) ,
wadau wa maendeleo kutoka Jumuiya ya Ulaya, mashirika yasiyo ya kiserikali
(NGOs) na wasomi.
Dkt. Kida
alisema, Majadiliano hayo nimatokeo ya juhudi zilizoanza tangu 1998-200, ambapo ESRF ilishiriki katika
uanzishwaji wa mpango wa Taifa wa Vision 2025 uliolenga kuitoa Tanzania kwenye
kundi la nchi masikini hadi zile zenye uchumi wa Kati, (Middle income coutry.
“Mwaka 2011
ESRF ilifanya mkakati wa kupitia mpango huo wa vision 2015 na kubaini masuala
kadhaa ambayo yalihitaji kuelezewa kama kweli taifa linaelewa mpango huo wa
kipindi kirefu.” Alisema na kuongeza ni hivi karibuni sisi katika ESRF
tulifanya mapitio ya mkakatiwa kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDPI), na
MKUKUTA II, mapitio ambayo yamechangia kuingia katika Mpango huu wa pili wa
Maendeleo wa Miaka Mitano, (FYDP II), Alisema Mkurugenzi huyo Mtendaji wa ESRF.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Tume ya
Mipango, kutoka Wiraza ya Fedha na Mipango, Dkt. Maduka Paul Kessy alisema, “Kuna
mambo matatu muhimu ya kuzingatia katika mkakati huu ambayo wajumbe mtalazimika
kuyafanyia kazi kwa kina ambayo ni pamoja na kutambua kwamba nchi yetu imedhamiria
kuingia kwenye uchumi wa viwanda, kwa hivyo rasilimali tulizonazo tuhakikishe
zinalisha viwanda vyetu mfano tunapaswa tujadiliane ni kwa namna gani tunafikia
hatua ya kuchakata pamba na ngozi hapa hapa nchini, na utengenezaji wa madawa.”,
aliwaambia washiriki wa warsha hiyo.
Ili
kutekeleza hilo, Viongozi wa Wilaya na Mikoa hawana budi kushirikiana na sekta
binafsina kujadili namna ya kutekeleza maswala haya ili kusudi ifikapo mwishoni
mwa Novemba mwaka huu, tutakapokutana tujue nini kilicho mbele yetu,
alifafanuaDkt. Kessy.
Akitoa
mada yake kuhusu ushirikishwaji wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi, Mkuu
wa mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka alisema, “Wakati umefika sasa, watanzania
kuanzisha viwanda vidogo vya kuongeza thamani ya mazao na mifugo ili kuboresha
maisha na kuondokana na tatizo la vijana kukosa kazi.
Akitolea
mfano, Mkuu huyo wa mkoa ambaye ameteuliwa na Rais John PombeMagufuli kuogoza
mkoa huo akitokea wilayani Mvomero mkoani Morogoro, alisema. “Sisi Simiyu
tumepiga hatua, hivi sasa tunatengeneza chaki sisi wenyewe kwa matumizi ya
shule, na tunataka pamba tunayolima ambapo Simiyu ndio mkoa unaoongoza kwa
uzalishaji wa zao hilo, tuanze kutengeneza vifaa vya hospitalini vinavyotokana
na zao la pamba. “ Alifafanua Mkuu huyo wa Mkoa kijana.
Bw.
Mtaka pia alisema, asilimia 50 ya mifugo inatoka mkoani Simiyu na moja ya
mkakati alioufanya kuwashirikisha SIDO na wadau wengine katika kuanzisha
kiwanda kidogo cha kuongeza thamani ya maziwa na kutengeneza bidhaa mbalimbali zitokanazo
na maziwa na nia yetu ni kusambaza viwanda vya aina hii kwenye kila wilayani
No comments:
Post a Comment