October 26, 2016

WAZIRI MBARAWA AMEITAKA BODI MPYA YA SHIRIKA LA POSTA KUSIMAMIA MAPATO

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Shirika la Posta.

Na Daudi Manongi, MAELEZO

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi  teule ya Shirika la Posta kutumia fursa zilizopo ili kuongeza vyanzo vya mapato vya Shirika hilo.
Profesa Mbarawa ameyasema hayo wakati akizindua Bodi mpya ya wakurugenzi ya Shirika la Posta katika ukumbi wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano leo Jijini Dar es Salaam.

“Nashukuru kwa kuwa mmekubali uteuzi wangu,mmekuja katika shirika zuri na hivyo kama mtajipanga mtaweza kufanya mambo mengi makubwa,naitaji mtu anayeweza kutafta mapato na shirika hili la Posta lina vyanzo vingi  lakini bado halijatumika vizuri na hivyo naomba mbadilishe mtazamo wa watu wetu ili msonge mbele” Alisema Prof Mbarawa.

Aidha Waziri Mbarawa ameitaka bodi iyo kuisimamia vizuri menejimenti ya Shirika la Posta ili ifanye kazi kwa ufanisi mkubwa na pia amemuagiza mwenyekiti wa bodi hiyo ya wakurugenzi kuwekeana mkakati wa mikataba ya kazi na malengo ili kupata matokeo mazuri  na amesisitiza kuboreshwa kwa mahusiano kati ya watendaji wa juu na wafanyakazi wa chini.

Waziri Mbarawa ameagiza bodi iyo teule  kusimamia huduma mpya ya Posta mlangoni na Huduma Center kwa uadilifu ili vilete tija kama ilivyokusudiwa na kuihakikishia bodi iyo kuwa serikali imejipanga  kulipa Deni la kampuni iyo ili kupunguza mzigo wa utendaji wa shirika hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Luteni kanali Msaafu Haruni Kondo amemhakikishia waziri uyo kuwa wataisimamia vyema menejimenti ya Shirika hilo  na kuhakikisha vyanzo vya mapato vinapatikana kama alivyoagiza kwani utekezaji wa majukumu ndio msingi wa maendeleo wa shirika hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages