Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Shirika la Posta.
Na Daudi Manongi, MAELEZO
Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi teule ya Shirika la Posta kutumia fursa
zilizopo ili kuongeza vyanzo vya mapato vya Shirika hilo.
Profesa Mbarawa
ameyasema hayo wakati akizindua Bodi mpya ya wakurugenzi ya Shirika la Posta
katika ukumbi wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano leo Jijini Dar es
Salaam.
“Nashukuru kwa kuwa
mmekubali uteuzi wangu,mmekuja katika shirika zuri na hivyo kama mtajipanga
mtaweza kufanya mambo mengi makubwa,naitaji mtu anayeweza kutafta mapato na
shirika hili la Posta lina vyanzo vingi lakini bado halijatumika vizuri na hivyo
naomba mbadilishe mtazamo wa watu wetu ili msonge mbele” Alisema Prof Mbarawa.
Aidha Waziri Mbarawa
ameitaka bodi iyo kuisimamia vizuri menejimenti ya Shirika la Posta ili ifanye
kazi kwa ufanisi mkubwa na pia amemuagiza mwenyekiti wa bodi hiyo ya
wakurugenzi kuwekeana mkakati wa mikataba ya kazi na malengo ili kupata matokeo
mazuri na amesisitiza kuboreshwa kwa
mahusiano kati ya watendaji wa juu na wafanyakazi wa chini.
Waziri Mbarawa
ameagiza bodi iyo teule kusimamia huduma
mpya ya Posta mlangoni na Huduma Center kwa uadilifu ili vilete tija kama
ilivyokusudiwa na kuihakikishia bodi iyo kuwa serikali imejipanga kulipa Deni la kampuni iyo ili kupunguza
mzigo wa utendaji wa shirika hilo.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Luteni kanali Msaafu
Haruni Kondo amemhakikishia waziri uyo kuwa wataisimamia vyema menejimenti ya
Shirika hilo na kuhakikisha vyanzo vya
mapato vinapatikana kama alivyoagiza kwani utekezaji wa majukumu ndio msingi wa
maendeleo wa shirika hilo.
No comments:
Post a Comment