MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akishiriki kwenye mazoezi hayo kwa ajili ya kuimarisha miili yao na kujenga afya.
MKUU wa wilaya ya Muheza
Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akishiriki mazoezi ya
kuruka ikiwa ni kuunga mkono agizo la
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu
leo kwenye uwanja wa
Jitegemee wilayani Muheza
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akishiriki kwenye kukumbia ikiwa ni kufanya Jogging inayofanyika kila mwezi wilayani humo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza, Desderia Haule wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akiteta jambo na Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew mara baada ya kumalizika mazoezi hayo. |
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa Jogging hiyo. |
MKUU wa Wilaya ya Muheza
Mhandisi Hajat Mwanasha Tumbo amewaagiza watendaji wa kata na Vijiji kuhakikisha wanatenga
maeneo ya viwanja vya
michezo ili kuwezesha vijana kushiriki kwenye michezo jambo
ambalo linaweza kuwasaidia
kupata ajira na kuweza kujikwamua kimaisha.
Agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo alilitoa leo wakati akiunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais Samia Suluhu ya kufanya mazoezi kila Juma mosi ya pili ya mwezi lengo likiwa kuimarisha afya na miili ya watumishi na vijana ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo yanaweza kuwanyemelea.
Alisema kutokuwepo kwa viwanja vya kutosha Wilayani humo kunapunguza fursa kwa wananchi na vijana wengi kutokufanya mazoezi na hata kuonyesha vipaji vyao ambavyo vingeweza kuwa sehemu ya kujipatia ajira.
“Michezo ni afya na ajira,kuongeza idadi ya viwanja kutatuongezea
mchango mkubwa wa kukuza vipaji na kufungua fursa za ajira kwa vijana wengi ambao asilimia kubwa wapo mtaani wakiwa wanakabiliwa na ugumu wa maisha”Aliseam Hajat Tumbo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo (DMO) Mathew Mganga alisema kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la magonjwa wa magonjwa yasiyoambukizwa kutokana na kutokuwepo na utaratibu wa kufanya mazoezi hasa kwa watumishi wa Serikali.
Alisema ili kuweza kukabiliana
na magonjwa hayo
yasiyoambukizwa kama
ugonjwa wa Moyo,sukari na shindikizo la damu lazima kauli ya
makamu wa Rais ya kuhamasisha
kufanyike mazoezi nchi nzima itekelezwe kwa vitendo na si maneno.Agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo alilitoa leo wakati akiunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais Samia Suluhu ya kufanya mazoezi kila Juma mosi ya pili ya mwezi lengo likiwa kuimarisha afya na miili ya watumishi na vijana ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo yanaweza kuwanyemelea.
Alisema kutokuwepo kwa viwanja vya kutosha Wilayani humo kunapunguza fursa kwa wananchi na vijana wengi kutokufanya mazoezi na hata kuonyesha vipaji vyao ambavyo vingeweza kuwa sehemu ya kujipatia ajira.
“Michezo ni afya na ajira,kuongeza idadi ya viwanja kutatuongezea
mchango mkubwa wa kukuza vipaji na kufungua fursa za ajira kwa vijana wengi ambao asilimia kubwa wapo mtaani wakiwa wanakabiliwa na ugumu wa maisha”Aliseam Hajat Tumbo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo (DMO) Mathew Mganga alisema kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la magonjwa wa magonjwa yasiyoambukizwa kutokana na kutokuwepo na utaratibu wa kufanya mazoezi hasa kwa watumishi wa Serikali.
“Laima tubadilike kwa kufanya mazoezi ili kupunguza magonjwa hayo ambayo yamekuwa pigo kwa wananchi na hasa watumishi wa Umma,inatulazimu tupambane kukabiliana na hali hiyo kwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuboresha afya zetu”Alisema Dk Mathew.
Naye Katibu Tawala Wilaya hiyo Desderia Haule ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Wilya alisema zoezi hili litakuwa ni endelevu na Serikali itatenga maeneo ya kutosha ya viwanja kwa ajili mazoezi na kukuza vipaji vya vijana . Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
No comments:
Post a Comment