January 15, 2017

TASWA YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO, AMINA ATHUMAN

Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), kimepokea kwa mshtuko taarifa za kifo cha mwanachama wake, Amina Athuman (wa kwanza kulia) kilichotokea leo katika hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar. 

'Tunaungana na kuwapa pole familia ya marehemu na wadau wengine katika tasnia katika kipindi hiki kigumu cha majonzi', 

Taratibu zingine zitatolewa baadae kadir zitakavyokuwa zikipatikana ilisema taarifa ya Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando. 


Amina alilazwa hospitalini hapo baada ya kuzidiwa (kushikwa na uchungu) kutokana na ujauzito na kukimbizwa kupata huduma katika hospitali hiyo ambapo alijifungua mtoto wa Kiume (Bahati mbaya) na yeye akaendelea kupatiwa matibabu hadi ulipomkuta umauti asubuhi ya leo.

Amina alikua mjini Zanziba kikazi kuripoti mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo alikuwa arejee jijini Dar es Salaam jana.


No comments:

Post a Comment

Pages