Mwenyekiti wa Kitengo cha
Nafaka na Mamalishe wa Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam, Bw. Mohamed Salum akielezea jambo kwa mwandishi
wa habari kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula katika Soko hilo leo jijini Dar
es Salaam. Mohamed amesema kuwa chakula kinapatikana kwa wingi kutoka maeneo
mbalimbali ya mikoa.
Picha ikionyesha baadhi ya nafaka zikiwa zinauzwa katika Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya nafaka zikiwa zinauzwa katika Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam.
KS3: Mkazi wa jijini Dar es Salaam akinunua nafaka katika Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam leo. Picha na: Frank Shija – MAELEZO.
Na Frank Shija – MAELEZO
HALI ya upatikanaji wa chakula nchini
inaridhisha licha ya changamoto ya kuongezeka kwa bei ya bidhaa za chakula
zitokanazo na nafaka.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti
wa Kitengo cha Nafaka na Mamalishe wa Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam,
Bwana Mohamed Salum katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii leo
jijini Dar es Salaam.
Mohamed amesema kuwa pamoja na
kuwa Dar es Salaam inategemea chakula kutoka mikoani bado hali ya upatikanaji
wake ni mkubwa na wa kuridhisha kama ambavyo imekuwa miaka ya nyuma.
“Chakula bado kinapatika kwa wingi
japo changamoto iliyopo ni ongezeko la bei pekee kitu ambacho si kigeni duniani
kote,” alisema Salum.
Alisema nia ajabu sana kusikia
watu wanasema kuna baa la njaa wakati vyakula vinapatikana kwa wingi katika
masoko yetu.
Aliongeza kuwa kungekuwa na tatizo
la uhaba wa chakula basi hata uingizwaji wa chakula katika jiji la Dar es
Salaam ungepungua kwani asilimia kubwa inategemea chakula kutoka mikoani,
badala yake upatikanaji wa chakula umeendelea kuwa wa kuridhisha.
“Ndugu mwandishi ukitaka kujua
kuwa hakuna uhaba wa chakula jaribu kutembelea maeneo ya Manzese Uzuri
utajionea namna maroli matani kwa matani yanayoingiza nafaka kwenye mashine za
kusaga na kukoboa.” Alisisitiza.
No comments:
Post a Comment