January 22, 2017

MH ANASTAZIA WAMBURA AONGOZA MAZOEZI IRINGA

Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura leo ameongoza wananchi wa Mkoa wa Iringa katika mazoezi ya kupambana na magonjwa kama kisukari na shinikizo la damu.

 Mazoezi hayo ambayo yalianzaia ofisi ya mkuu wa mkoa yalishirikisha viongozi, watumishi wa taasisi mbalimbali pamoja wanachi. 

Akimkaribisha Mh. Waziri Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza alimshukuru Mheshimiwa waziri kwa kutenga muda wake kuja kujumuika na wana Iringa. 

Akihitimisha mazoezi hayo Mh wambura alisisitiza suala la lishe bora na kuwaasa watanzania kugeuza mazoezi kuwa utamaduni. “ Kila mtanzania popote alipo aanze sasa kuona mazoezi ni moja ya mila na desturi yake au utamaduni”

Mkuu wa wilaya ya Iringa alisisitiza kuwa mazoezi hayo yataendelea kila jumamosi kasoro jumamosi ya usafi. Tarehe 4/2/2017 mazoezi haya yatafanyika tena ambapo anatarajiwa kualikwa Mh Ummy Mwalimu kuja kushiriki mazoezi.

Wananchi wa rika mbali mbali walitembea pamoja na viongozi wa mkoa na wilaya. Akihojiwa kamanda wa Polisi wa Mkoa Kamishna Msaidizi wa Polisi Mjengi alisema amaefarijika kuona mwamko wa mazoezi “ sisi tunafanya mazoezi karibu kila siku mwamko huu ukiendelea Iringa hakuta kuwa na magonjwa kabisa pia itawajenga wananchi kujilinda na uhalifu.”
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mh. Richard Kasesela (kulia), akiwa na RPC wa Iringa wakishiriki katika mazoezi ya katika mazoezi ya kupambana na magonjwa kama kisukari na shinikizo la damu. 
Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura (wa pili kushoto), akiongoza wananchi katika mazoezi ya kupambana na magonjwa kama kisukari na shinikizo la damu.

No comments:

Post a Comment

Pages