Sehemu ya maduka yaliyoungua moto jijini Arusha leo. (Picha na Grace Macha).
NA GRACE MACHA, ARUSHA
MADUKA matano yameteketezwa kwa moto maeneo ya mianzini jijini hapa baada ya kutokea hitilafu ya umeme iliyosababisha majokofu yaliyokuwa kwenye super market iliyo kwenye jengo hilo kushika moto.
Moto huo ulianza leo majira ya saa 12 asubuhi ambapo uliteketeza kabisa bidhaa zilizokuwa kwenye super market hiyo na maduka manne ya jirani kutokana na mitungi ya gesi ya kuuza iliyokuwa karibu kulipuka hivyo kuufanya uzidi kuwa mkubwa.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, (RPC), Charles Mkumbo, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa
nyumba hiyo inamilikiwa na ndugu wawili , Emanuel Hagai na Benjamin Hagai.
Alisema hasara ikiyotokana na tukio hill bado haijajulikana ambapo bado wanaendelea kujua chanzo halisi kwani taarifa za awali zinaonyesha chanzo ni hitilafu ya umeme.
Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo, Julius Mollel alisema kuwa moto huo ulikuwa mkubwa sana hasa sehemu ya mbele kulipokuwa na mitungi ya gesi.
Alisema kuwa hats gari la kuzima moto lilipofika eneo hilo iliwawia vigumu kuuzima hivyo wakawa wanazima kuzunguka eneo hilo ili kuuzuia usisambae zaidi.
Hata hivyo mtaalam mmoja wa masuala ya moto ambaye hakupenda jina lake kiandikwe gazetini alisema kuwa inawezekana watu wa zimamoto hawakuuzima moto huo eneo lenye gesi kutokana na moto huo kuwa na dawa tofauti ya kuuzima.
No comments:
Post a Comment