January 24, 2017

MSIMU WA PILI WA MRADI WA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI KUPITIA TAASISI YA "MANJANO FOUNDATION"

Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation utaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Mtwara, Tabora na Kigoma kwa mwaka 2017. Mafunzo hayo yatatolewa kwa Wanawake watakaotuma maombi na watakaochaguliwa katika Mikoa hiyo husika. 

Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa mwaka mmoja kwa lengo la kuhakikisha wanafikia malengo yao waliojiwekea. Wanawake wakazi wa mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Mtwara, Tabora na Kigoma wanaopenda kunufaika na mradi huo wanaombwa kutuma maombi na kujisajili kupitia Tovuti ya http://www.manjanofoundation.org/


Mafunzo hayo yana lengo la kumsaidia mjasiriamali Mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato kupitia Tasnia ya Vipodozi. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha, muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 

Awamu ya pili ya mafunzo hayo itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano na elimu ya ngozi.

No comments:

Post a Comment

Pages