![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhvNIgkEsrBK3XQY0zXFIHvLLpAj1YObeFMdfDE3knVvWWQVyuNEqdAiwmMgu5jgs6yTkqoBUmTxkXuzl6P9NTEy9VagTFTecq4awqZKul4x9pycV-i1PONSvNQ_HIDLFm9r3VGVdbC9qE/s640/DG_PSPF.jpg)
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF, umeendesha semina ya mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Katibu
Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, ili kuwajengea uwezo wa kushughulikia matatizo ya
wananchi ambao ni wanachama wa Mfuko huo.
Mafunzo
hayo ya siku mbili, yameanza leo Januari 3, 2017, na kufunguliwa na Katibu
Tawala Msaidizi (sehemu ya serikali za mitaa), Bi. Merry Assey kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa ea Dar es Salaam, Paul Makonda.
“Niipongeze
PSPF kwa kuandaa semina hii ambayo inatoa fursa ya watumishi hawa waliohudhuria
katika mafunzo haya kuelewa huduma na shughuli zinazofanywa na Mfuko huu na kwa
maana hiyo iwe rahisi kwenu kutatua kero za wananchi wanaofika pale Ofisini kwa
Mkuu wa Mkoa kutafuta ufumbuzi hususan kwa wanachama wa Mfuko huu,.” Alisema
Bi. Assey, wakati akifungua semina hiyo.
Akimkaribisha
mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, alisema, PSPF ilifikia
uamuzi wa kuandaa semina hiyo kufuatia wazo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
ambaye alitaka kujengewa uwezo kwa watumishi wa Ofisi yake ili waweze
kuwahudumia vema wananchi wakiwemo wanachama wa PSPF.
“Nililipokea
wazo hilo na sisi PSPF tukaona ni fursa nzuri kwa kuwaelimisha watumishi hawa
ambao, ninahakika baada ya mafunzo haya, watakuwa mabalozi wetu wazuri lakini pia
na wao watajiunga na Mfuko huu.” Alisema Bw. Mayingu.
Mada
mbalimbali zilitolewa kwa wanasemina hao ikiwa ni pamoja na ile ya shughuli za
Mfuko iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma wa Mfuko huo, Bi. Neema Muro, Kaimu
Meneja Mafao, Bw. Haji Moshi na Maafisa wengine wa Mfujko huo.
No comments:
Post a Comment