Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli leo Jumapili Januari Mosi, 2017 ameendelea na ziara yake ya siku mbili
Mkoani Kagera kwa kukagua na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha afya
cha Kabyaile kilichopo Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera
Akizungumza na wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi
wa kituo hicho cha Afya Rais Dkt Magufuli amesema serikali kwa sasa imeweka
nguvu kubwa katika kurejesha miundo mbinu ya huduma za jamii iliyoharibiwa na
tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10,2016 Mkoani humo badala ya kujenga
nyumba ya mwananchi mmoja mmoja.
''Na ndio maana nimeona
leo hapa tarehe moja mwezi wa kwanza mwaka 2017 niwaeleze ukweli maana kuna
watu wanapitapita huko na wapo wengine nyumba zao zilibomoka kidogo
wakadanganywa wakaambiwa kuwa serikali itakuja kuwajengea nyumba wakazibomoa
zote ''waafwa'' kama ulitegemea ukiibomoa utalipwa fidia,hakuna''
Aidha Dkt Magufuli amemwagiza Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo kupeleka huduma ya umeme katika kituo hicho cha
afya alichokiwekea jiwe la msingi,ambapo pia ameahidi kutoa kiasi cha shilingi
Bilioni moja kwa ajili kutengeneza barabara inayoelekea kituoni hapo kwa
kiwango cha lami.
Pia ameuagiza uongozi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) wanaojenga kituo hicho cha afya kuharakisha ujenzi wake na kukamilika
kabla ya mwezi februari badala ya Machi mwaka huu.
Dkt Magufuli ameutaka uongozi na wananchi wa Wilaya ya
Misenyi na maeneo mengine nchini kutumia vyema mvua chache zinazonyesha mkoani
humo kulima mazao yanayokomaa kwa muda mfupi ili kuepukana na baa la njaa na
kwamba serikali haina mpango wa kugawa chakula cha bure.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais, IKULU
Kagera.
01 Januari, 2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha
wageni mara baada ya kuwasili katika eneo la Ujenzi wa Kituo cha Afya cha
Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera.
Picha namba 2. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera. Wengine katika picha ni Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Vija Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako wakiwa wameshika utepe huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
Taaswira ya moja ya jengo katika mradi huo wa kituo cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment