Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

NA MWANDISHI
WETU
MWIMBAJI wa
kimataifa wa nyimbo za injili, Pastor Solly Mhalangu kutoka nchini Afrika Kusini, amethibitisha
kushiriki Tamasha la Pasaka linaloadhimisha miaka 17 tangu kuasisiwa kwake mwaka
2000 chini ya uratibu wa kampuni ya Msama Promotions.
Solly ambaye
amekuwa king’ara vilivyo katika muziki wa injili kama mwimbaji anayejipambanua
na wengine kama mchangamshaji zaidi jukwaani, pia ni kiongozi wa kanisa nchini
Afrika Kusini , hivyo kuenfesha huduma zote mbili kila moja kwa wakati wake.
Alex Msama, Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo litakalozinduliwa April 16, mwaka huu
katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea katika mikoa
mingine mitano, alisema jana kwamba mwimbaji huyo amethibitisha kushiriki tukio
hilo lenye kubeba hadhi na vionjo vya kimataifa.
“Nikiwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, nina furaha kubwa
kusema kuwa mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili kutoka nchini Afrika Kusini,
amethibitisha kushiriki tamasha la
Pasaka la mwaka huu litakalofanyika katika mikoa sita ikiwemo Dar es Salaam,”
alisema.
Alisema ujio
wa Mahlangu katika tamasha hilo, kunafanya maandalizi ya Tamasha hilo yazidi
kuimarika kutokana na umaarufu wa mwimbaji huyo anayesifika ndani na nje ya
Afrika Kusini kwa huduma ya uimbaji wa nyimbo zenye ujumbe wa kuvutia wengi na
kuchangamsha jukwaa.
Msama
alisema kwa vile si mara ya kwanza kwa Mahlangu kushiriki Tamasha la Pasaka,
wadau na wapenzi wa Tasmaha hilo wajitokeze kwa wingi kuja kufaidi Baraka za
Mungu kupitia ujumbe wa Neno la Mungu kutoka kwa mwimbaji huyo na wengine kibao
akiwemo malkia wa muziki wa injili Afrika Mashariki, Rose Muhando.
Alisema
Mahlangu ambaye atakuwa na kundi lake, atashirikiana na waimbaji wengine
walitangazwa tayari ambao tayari wapo katika maandalizi ya nguvu kwa lengo la
kutoa huduma bora siku hiyo ya uzinduzi wa Tamasha hilo lenye kubeba maudhui ya
kueneza ujumbe wa neno la Mungu na sehemu ya mapato kusaidi makundi maalumu.
Msama alisema
Tamasha la mwaka huu litabeba uzinduzi wa albamu mbili; moja ya Muhando
inayoitwa Jitenge na Ruth pamoja na
albamu mpya ya Kwaya ya Kinondoni Revival ya jijini Dar es Salaam, iitwayo
‘Ngome Imeanguka.’
No comments:
Post a Comment