HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 24, 2017

TBL GROUP YASHIRIKI KAMPENI YA KUWAJENGEA WASICHANA UWEZO

Meneja wa Mawasiliano wa TBL Group, Zena Tenga, akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Premier iliyopo Bagamoyo katika semina ya kuwajengea uwezo wa kujiamini na kukabiliana na changamoto mbalimbali chini ya mpango unaojulikana kama HerAfrica.
Wanafunzi wasichana wa shule ya sekondari ya Premier iliyopo Bagamoyo katika picha ya pamoja wakati wa semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na mpango wa HerAfrica.


Kampuni ya TBL Group imeelezea dhamira yake ya kuunga mkono serikali na taasisi mbalimbali zinazotekeleza mpango wa kuwajengea uwezo watoto wa kike na kuwasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili na kusababisha wabaki nyuma.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Masuala yanayohusiana na kampuni wa TBL Group, Georgia Mutagahywa,aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akieleza jinsi kampuni ilivyoshiriki katika semina ya mpango wa kuzungumza na wasichana kuhusiana kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili ujulikanao kama HerAfrica.

“Mtazamo wetu ndani ya kampuni suala la jinsia tunalipa umuhimu mkubwa kwa kuwa tunaamini kuwa wanawake wanao uwezo wa kufanya vizuri wakipata fursa na kuondokana na changamoto zinazosababisha wabaki nyuma na tutaendelea kuunga mkono jitihada za serikali na taasisi mbalimbali zinazopambana na usawa wa kijinsia na kuondokana na mila potofu zinakwamisha wanawake na kusababisha wabaki nyuma” alisema Mutagahywa.

Katika semina ya taasisi ya HerAfrica iliyofanyika katika sekondari ya wasichana ya Premier iliyopo Bagamoyo, Meneja wa Mawasiliano wa TBL Group, Zena Tenga ,aliungana na wanawake wengine kutoa mada za kuwajengea uwezo wa kujiamini wasichana wanaosoma katika shule hiyo.

Mbali na mada za kuwajengea uwezo wa kuamini pia wanafunzi hao wasichana walielezwa changamoto mbalimbali wanazoweza kukutana nazo katika ujana wao zinazoweza kupelekea kushindwa kutimiza ndoto zao na walipewa mbinu na mikakati ya kuzikabili ili waweze kutumiza ndoto zao pia walielezwa umuhimu wa kujibidiisha na masomo yao kwa kuwa elimu ni silaha pekee itakayoweza kuwakomboa.

Mratibu wa programu hiyo nchini,Lilian Matari,kutoka kampuni ya Ushauri wa kitaalamu ya LAS alisema kuwa hii ni semina ya pili ya kuongea na wasichana kufanyika na mkakati wa kampuni ni kuendesha semina nyingi nchini kote ili kuwafikia wasichana wengi hususani waliopo mashuleni.

No comments:

Post a Comment

Pages