HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 22, 2017

TRA Yatoa siku 39 kodi ya majengo iwe imelipwa Mwanza

Kamishna Mkuu wa TRA nchini,Charles Kichere, akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza)

Na Atley Kuni- Afisa habari Mwanza.

Mamlaka ya mapato nchini imetoa muda hadi kufikia Juni 30, mwaka huu wananchi wote wanaodaiwa kodi ya majengo kuhakikisha wanailipa kodi hiyo ilikuepuka kufikishwa mahakamani na kutozwa faini.

Kauli hiyo imetolewa na kamishina mkuu wa TRA nchini ndugu Charles Kichere, alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza hii leo.

“Mwisho wa kulipa kodi ya majengo bila adhabu ni tarehe 30 Juni, 2017. Hivyo wenye majengo yaliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), na Manispaa ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo karibu nao kuchukua ankara zao endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa yao au kujisajili na kulipa kupitia benki yoyote ya biashara” alisema Kichere. 

Kichere amefafanuakuwa kwa walioko sehemu ambazo nyumba zimethaminishwa watalipa kiwango cha asilimia ya thamani ya jengo kama inavyoonesha kwenye ankara zao na walioko maeneo ambayo hayajapimwa au kuthaminishwa watalipa viwango maalum vilivyopitishwa na mabaraza ya madiwani na kutangazwa na TRA kwenye vyombo vya habari.

Kichere amevitaja viwango hivyo vilivyopitishwa kuwa, ni shilingi za kitanzania (20,000) kwa Jiji la Mwanza na kumi na tano elfu (15,000) kwa Manispaa ya Ilemela. 

TRA pia imepongeza ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na safu yake nzima ya uongozi ikiwemo Serikali za Mitaa husika. “Mhe mkuu wa Mkoa ushirikiano huo umetuwezesha kutoa makadirio sahihi ya tozo, kutumia viwango rafiki, kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji, Kutoa elimu kwa jamii, kushughulikia pingamizi za kodi ya majengo kwa wakati na kuendelea kuimarisha uthamini wa majengo” amesema Kichere.

Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema katika kufikia adhma hiyo ya ukusanyaji mapato, wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa huo hawataruhusiwa kutoka nje ya vituo vyao vya kazi hadi kuisha kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017. “Ajenda yetu kuu ni kukusanya Mapato, hivyo Ndugu kamishna mimi nikuthibitishie tu kuwa kwa sasa, hatuta ruhusu Mkurugenzi atoke katika kituo chake cha kazi labda kama amepata Msiba” amesema Mongella.

TRA Yatoa siku 39 kodi ya majengo iwe imelipwa Mwanza.

Mamlaka ya mapato nchini imetoa muda hadi kufikia Juni 30, mwaka huu wananchi wote wanaodaiwa kodi ya majengo kuhakikisha wanailipa kodi hiyo ilikuepuka kufikishwa mahakamani, kutozwa faini au vyote viwili.

Kauli hiyo imetolewa na kamishina mkuu wa TRA nchini ndugu Charles Kichere, alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza hii leo.

“Mwisho wa kulipa kodi ya majengo bila adhabu ni tarehe 30 Juni, 2017. Hivyo wenye majengo yaliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), na Manispaa ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo karibu nao kuchukua ankara zao endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa yao au kujisajili na kulipa kupitia benki yoyote ya biashara” alisema Kichere. 

Kichere amefafanuakuwa kwa walioko sehemu ambazo nyumba zimethaminishwa watalipa kiwango cha asilimia ya thamani ya jengo kama inavyoonesha kwenye ankara zao na walioko maeneo ambayo hayajapimwa au kuthaminishwa watalipa viwango maalum vilivyopitishwa na mabaraza ya madiwani na kutangazwa na TRA kwenye vyombo vya habari.

Kichere amevitaja viwango hivyo vilivyopitishwa kuwa, ni shilingi za kitanzania (20,000) kwa Jiji la Mwanza na kumi na tano elfu (15,000) kwa Manispaa ya Ilemela. 

TRA pia imepongeza ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na safu yake nzima ya uongozi ikiwemo Serikali za Mitaa husika. “Mhe mkuu wa Mkoa ushirikiano huo umetuwezesha kutoa makadirio sahihi ya tozo, kutumia viwango rafiki, kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji, Kutoa elimu kwa jamii, kushughulikia pingamizi za kodi ya majengo kwa wakati na kuendelea kuimarisha uthamini wa majengo” amesema Kichere.

Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema katika kufikia adhma hiyo ya ukusanyaji mapato, wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa huo hawataruhusiwa kutoka nje ya vituo vyao vya kazi hadi kuisha kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017. “Ajenda yetu kuu ni kukusanya Mapato, hivyo Ndugu kamishna mimi nikuthibitishie tu kuwa kwa sasa, hatuta ruhusu Mkurugenzi atoke katika kituo chake cha kazi labda kama amepata Msiba” amesema Mongella TRA Yatoa siku 39 kodi ya majengo iwe imelipwa Mwanza.

Mamlaka ya mapato nchini imetoa muda hadi kufikia Juni 30, mwaka huu wananchi wote wanaodaiwa kodi ya majengo kuhakikisha wanailipa kodi hiyo ilikuepuka kufikishwa mahakamani, kutozwa faini au vyote viwili.

Kauli hiyo imetolewa na kamishina mkuu wa TRA nchini ndugu Charles Kichere, alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza hii leo.



“Mwisho wa kulipa kodi ya majengo bila adhabu ni tarehe 30 Juni, 2017. Hivyo wenye majengo yaliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), na Manispaa ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo karibu nao kuchukua ankara zao endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa yao au kujisajili na kulipa kupitia benki yoyote ya biashara” alisema Kichere. 

Kichere amefafanuakuwa kwa walioko sehemu ambazo nyumba zimethaminishwa watalipa kiwango cha asilimia ya thamani ya jengo kama inavyoonesha kwenye ankara zao na walioko maeneo ambayo hayajapimwa au kuthaminishwa watalipa viwango maalum vilivyopitishwa na mabaraza ya madiwani na kutangazwa na TRA kwenye vyombo vya habari.

Kichere amevitaja viwango hivyo vilivyopitishwa kuwa, ni shilingi za kitanzania (20,000) kwa Jiji la Mwanza na kumi na tano elfu (15,000) kwa Manispaa ya Ilemela. 

TRA pia imepongeza ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na safu yake nzima ya uongozi ikiwemo Serikali za Mitaa husika. “Mhe mkuu wa Mkoa ushirikiano huo umetuwezesha kutoa makadirio sahihi ya tozo, kutumia viwango rafiki, kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji, Kutoa elimu kwa jamii, kushughulikia pingamizi za kodi ya majengo kwa wakati na kuendelea kuimarisha uthamini wa majengo” amesema Kichere.

Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema katika kufikia adhma hiyo ya ukusanyaji mapato, wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa huo hawataruhusiwa kutoka nje ya vituo vyao vya kazi hadi kuisha kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017. “Ajenda yetu kuu ni kukusanya Mapato, hivyo Ndugu kamishna mimi nikuthibitishie tu kuwa kwa sasa, hatuta ruhusu Mkurugenzi atoke katika kituo chake cha kazi labda kama amepata Msiba” amesema Mongella 

Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua ni kwa namna gani TRA inaweza kufanya ili kurahisisha mfumo wa malipo kwakutumia mitandao ya simu, amesema wao kama TRA kila siku hupokea maoni ya wadau ili kuboresha shughuli zao na kwa hali hiyo wanaona ni wazo jema.

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA, pamoja na majukumu yake imeongezewa jukumu lakukusanya kodi za majengo ambapo mara baada yakukusanya kodi hizo, zitatolewa taarifa, lakini pia zitapelekwa kwenye Halmashauri husika kwa ajili ya shughuli za Maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Pages