Mdau wa Maendeleo, Boniface Myala akikabidhi daftari kwa Mwalimu wa Shule
ya Msingi Kunguru Goba, Sikujua Ramadhani leo jijini Dar es Salaam
Na: Mwandishi Wetu
Watanzania wametakiwa kuisaidia serikali katika kutatua
changamoto katika sekta mbalimbali ili kujiletea maendeleo kwa haraka badala ya
kusubiri kila jambo lifanywe na serikali.
Kauli hiyo imetolewa na Mdau wa Maendeleo Bw. Boniface Myalla
wakati alipotembelea shule ya Msingi Kunguru iliyopo Goba na kugawa Daftari kwa
wanafunzi 300 wa darasa la kwanza.
Myalla amesema, Watanzania hawana budi kuunga mkono jitihada
zinazofanywa na serikali inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli za
kuhakikisha inaleta maendeleo na huduma bora kwa wananchi.
"Serikali imetekeleza jukumu lake la kutoa elimu bure,
imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya wanafunzi kusoma bure, sasa imebaki upande
wetu wazazi na walezi kuwawezesha wanafunzi kupata vifaasaidizi," amesema.
Amesema lengo la kutoa madaftari hayo ni kuunga mkono serikali
ya Rais Dk. John Pombe Magufuli katika
dhamira yake ya kuhakikisha Tanzania mpya inajengeka, Tanzania ambayo kila
Mtanzania atanufaika na nchi yake lakini pia kupata elimu bora.
Akizungumza baada ya kupokea zawadi hizo, Mwalimu wa wanafunzi
hao, Sikujua Ramadhani amemshukuru Myala na kuiomba serikali na wadau wengine
kujitokeza na kutoa msaada ili kukamilisha malebgo na ndoto za wanafunzi.
Amesema wapo wanafunzi walikuwa wakishindwa kuandika kwa kukosa
madaftari na vifaa vingine vya kujifunzia hivyo ujio wa madaftari hayo
utapunguza kero changamoto hiyo.
No comments:
Post a Comment