Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania), Gift Shoko akizungumza na baadhi ya wateja wakubwa wa benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wakati benki hiyo ilipoandaa futari mahsusi. Kati ya mengi aliyoeleza, Shoko aliwahakikishia wateja wa benki hiyo jitihada madhubuti na endelevu zinazoendelea kufanya na benki ya CBA kwa kuboresha huduma na bidhaa zake wakati wote. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangala kama mgeni rasmi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania), Jijini Dar es Salaam.
Wateja wakubwa wa Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania), wakipakua futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Masoko wa Benki ya CBA Tanzania, Solomono Kawiche (wa kwanza kulia) akimuongoza na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla pamoja na Mke wake kupakua futari. Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania), Gift Shoko (wa kwanza kushoto) akipakua futari pamoja na wateja.
Wateja wakipata futari kwa pamoja.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania), Gift Shoko (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla pamoja na mteja wa CBA Benki.
No comments:
Post a Comment