Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (kushoto), akismikiliza Mwanachama wa Mfuko huo, Bw.Clemence Munisi, aliyefika kitengo cha huduma kwa wateja ili kuhudumiwa wakati wa kilele cha wiki ya utumishi Makao Makuu ya PPF Barabara za Samora/Morogoro jijini Dar es Salaam, Ijumaa Juni 23, 2017.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAKATI
siku ya Wiki ya Utumishi wa Umma imefikia kilele leo Juni 23, 2017, Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, aliiacha ofisi yake na
kujiunga na kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Mfuko huo Makao Makuu ya PPF barabara ya Samora na Morogoro jijini Dar es Salaam ambapo alifanya kazi ya
kuwahudumia wateja.
Awali
Bw. Erio alizungumza na baadhi ya wanachama wa Mfuko waliofika kwenye kitengo
hicho kuhudumiwa, na kusikiliza maoni yao ni jinsi gani wanahudumiwa na
Wafanyakazi wa Kitengo hicho.
Idha Mkurugenzi Mkuu Erio pia aliwahudumia wanachama wengine akiwemo mzee Clemence Munisi ambaye ni mstaafu wa kampuni ya Narco.
Idha Mkurugenzi Mkuu Erio pia aliwahudumia wanachama wengine akiwemo mzee Clemence Munisi ambaye ni mstaafu wa kampuni ya Narco.
Kwa
mujibu wa Mzee Munisi, yeye alisema, amefurahishwa na huduma zitolewazo na
Mfuko ambapo zimekuwa ni za haraka na zisizokuwa na usumbufu.
Baada
ya kutembelea kitengo hicho, Bw. Erio alikutana na baadhi ya wafanyakazi ili
kusikiliza maoni yao kuhusu namna uongozi wa Mfuko unavyoshirikiana na
wafanyakazi katika kulihudumia taifa.
“Kama
mjuavyo hii ni siku ya mwisho ya wiki ya utumishi, nimeona nikutane nanyi ili
kuwasikiliza, maana mara nyingi sisi viongozi ndio tunasema tu, lakini leo ni
zamu yenu ninyi watumishi kusema jambo lolote linalohusu Shirika letu, lakini
hata wewe binafsi kama mfanyakazi.” Alisema Bw. Erio.
Bw.
Erio pia aliwakumbusha wafanyakazi kuwajibika ipasavyo katika kuwahudumia
wananchi, lakini pia kuzingatia suala la afya bora.
“
Ili uweze kuwahudumia vema wananchi, ni lazima uwe na afya bora, mimi kama
mwenyekiti wa kamati ya UKIMWI ya shirika letu, bado nasisitiza, chukueni
tahadhari kubwa, kwani ugonjwa huu bado upo ingawa hauzungumzwi sana kwa sasa.”
Alionya Bw. Erio.
Bw
Erio pia aliwataka wafanyaakzi hao kutojihusisha kwa namna yoyote na matumizi
ya madawa ya kulevya au biashara ya madawa ya kulevya.
Mimi
siko serikalini, lakini ninao wajibu kama kiongozi wenu, kuwakumbusha mambo
ambayo jamii inapaswa kujiepusha nayo, na nyinyi kama sehemu ya jamii, hamna
budi kutojihusisha kwa namna yoyote na matumizi au biashara ya madawa ya
kulevya.” Alisema.
Kwa
upande wao wafanyakazi walishukuru uongozi wa Mfuko kwa kuwa karibu na
wafanyakazi. “Ukiona
hupati maneno mengi ujue mambo yako poa, sisi kwakweli tunashukuru sana kwa
kiongozi kama wewe kuja kusungumza nasi tena kwa kutusikilzia sisi tuna lipi la
ksuema, lakini nikuhakikishie tu kwa niaba ya vijana wenzangu, mimi naona mambo
yako safi na sikukuu hii tutasherehekea kwa furaha kabisa.” Alisema mfanyakazi
mmoja kutoma idara ya fedha, Bw.Joseph Fungo.
Naye
Meneja wa fedha wa PPF, Bw.Dozitte Msoffe, yeye alisema, mahusiano mema kati ya
uongozi na wafanyakazi ndiyo yanayoboresha utoaji huduma kwa wananchi na kwa
PPF, kumekuwepo na mahusiano mazuri sana baina ya pande hizi mbili kwa hivyo
mimi nikupongeze tu ndugu Mkurugenzi Mkuu, kwa uamjzi wako wa kuja kutusikiliza
hii huwezi kuisikia mahala pengine, lakini hapa PPF imetokea hongera sana.”
Alsiema Bw. Msoffe.
Bw. Erio akizungumza na baadhi ya wanachama waliofika kitengo cha huduma kwa wateja cha Mfuko huo ili kupaiwa huduma
Meneja wa Fedha wa PPF, Bw. Dozitte Msoffe akizungumza. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Lulu Mengele.
Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza Bw. Erio.
Bw. Msoffe akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. Erio na watumishi wengine wakimsikilizia
Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza Bw. Erio kwa makini
Afisa Fedha wa PPF, Bw. Joseph Fungo akizungumza
Baadhi ya wafanyakazi wakipiga makofi kufuatia mazungumzo mafupi ya Bw. Erio.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Bi. Gladness Mteta, (kulia) akiwa na Meneja wa Huduma za Utawala wa PPF, Bi. Cecilia Obeid Katikaza.
No comments:
Post a Comment