HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 06, 2017

MAELFU WAMZIKA NDESAMBURO

NA GRACE MACHA, MOSHI

Msafara wa magari uliokuwa ukiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe  uliwasili nyumbani hapo majira ya saa 9 alasiri ambapo mwili wa marehemu ulipelekwa moja kwa moja eneo lililoandaliwa kwa ajili ya maziko.

Ibada ya maziko ilianza nyumbani kwa marehemu Dkt Ndesamburo ikiongozwa na  Askofu Mkuu wa KKKT nchini, Dk. Frederick Shoo ambapo ilimalizika saa 9:30 ambapo zoezi la kuweka mashada ya maua lilianza likiwashirikisha wanafamilia, viongozi wa chama na Serikali waliofika.

SERIKALI YAWAKILISHWA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, William Lukuvi na mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba walihudhuria ibada ya mazishi kanisani na nyumbani.

Viongozi hao wa Serikali walishiriki shughuli hiyo ikiwa ni siku moja kushindwa kushiriki shughuli za kumuaga marehemu Ndesamburo kwenye viwanja vya majengo hali iliyoibua maswali miongoni mwa waombolezaji.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Mbowe aliwaeleza wananchi juzi kuwa kukosekana kwa uwakilishi wa Serikali haikuwa bahati mbaya bali ilikuwa ni hofu ya hatia.

"Wazungu wanamsemo kuwa wenye hatia wana hofu, kwahiyo kukosekana kwa uwakilishi wa serikali mahali hapa si ajabu wana hofu ya hatia,  nikupe pole dada yangu mbunge Mmasi (Esther wa CCM)  asante kwa kuja umejitahidi kufukia fukia kuipamba Serikali kwa kweli umejitahidi sana lakini ukweli ni serikali haina mwakilishi," alisema Mbowe huku waombolezaji wakipiga makofi.

Viongozi wengine walioshiriki ibada hiyo ya maziko na kuweka mataji ya maua kaburini waliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Mbowe, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Vicent Mashinji.

Wengine ni Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Makamu Mwenyekiti wa chama cha wananchi, (CUF), Severina Mwijage, Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Hashim Rungwe na Katibu Mkuu wa TADEA, John Shibuda.

Mbunge wa Moshi Mjini, Jafar Michael na Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya walipewa nafasi ya kuweka mashada  ambapo kutokana na wabunge na madiwani kuwa  wengi ilibidi mwakilishi mmoja kwa kila kundi aweke shada la maua kaburini kwa niaba yao.

Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi aliweka shada kwa niaba ya wafanyabiashara na wamiliki wa vyombo vya habari nchini.

Mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye na Waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba walipata fursa ya kuweka shada la maua.
 Jeneza lililokuwa na mwili wa muasisi wa Chadema marehemu Dk. Philemon Ndesamburo likiwa limefinikwa na bendera ya chama chake cha Chadema wakati wa mazishi yake leo.
Matayarisho ya kushusha jeneza katika nyumba yake ya milele. 
 Wanafamilia wakiwa katika mazishi ya Dk. Desamburo.
 Kuweka shada la maua. 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiweka shada la maua katika kaburi la muasisi wa Chadema, mzee Ndesamburo.

No comments:

Post a Comment

Pages