Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi ya mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2017/2018 Bungeni Mjini Dodoma.
Na Raymond Mushumbusi, Maelezo, Dodoma
Pato la kila mtanzania kwa mwaka 2016 limeongezeka kwa aslimia 11 kutoka shillingi 1,918,897 kwa mwaka 2015 mpaka kufikia shilling 2,131,299 kwa mwaka 2016.
Takwimu hizi zimebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango wakati akiwasilisha Bungeni Mjini Dodoma Taarifa ya Hali ya Uchumi ya mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2017/2018.
Akifafanua kuhusu ongezeko hilo Mhe. Dkt Philip Mpango amesema kuwa Pato la Taifa kwa mwaka 2016 lilifikia Shillingi million 103,744,606 kwa bei za mwaka husika na kiasi hiki kiligawanywa kwa idadi ya watu 48,676,698 walipo Tanzania Bara na kufanya wastani wa Pato la kila mtanzania kufikia kiasi cha Shillingi 2,131,299.
Ameeleza kuwa kwa thamani ya Dola za Marekani, wastani wa pato la Kila mtu liliongezeka kutoka Dola 967.5 mwaka 2015 hadi Dola 979.1 kwa mwaka 2016 ikionesha kuwa Tanzania inaelekea kwenye kundi la Uchumi wa kati.
“Serikali inaendelea kutatua changamoto mbalimbali ili tuweze kufikia Uchumi wa Kati kwa kuongeza fursa mbalimbali za uzalishaji nchini” alisistiza Mhe. Dkt Mpango.
Mhe. Dkt. Phili Mpango ameongeza kuwa Serikali imejipanga kuboresha shughuli za uzalishaji wa tija katika Sekta zinazoajiri hususan katika Sekta ya Kilimo cha mazao,Ufugaji na Uvuvi.
No comments:
Post a Comment