September 04, 2017

KAMPENI YA UZALENDO KWANZA YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR,KUHAMASISHWA NCHI NZIMA


Mwenyekiti wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza, Steven Mengele almaarufu kwa jina la kisanii Steven Nyerere, akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar kuhusina na uzinduzi wa kampeni yao itakayojulikana kwa jina la UZALENDO KWANZA. Pichani kulia ni Msanii wa Filamu Wastara na kulia kwake ni Misayo Ndumbagwe.

Kampeni hiyo imezinduliwa rasmi leo, ikiwa na lengo la kuunga mkono jitihada na juhudi zinazofanywa na Rais Dkt John Pombe Magufuli katika suala zima la kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kimaendeleo ambapo

wasanii wa muziki na filamu wapatao 250 wameshirkishwa pamoja na wachezaji wa mpira.
 
Steve amesema kuwa, ni wakati sasa kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuvienzi na kuvipenda vitu vyao kwa namna moja ama nyingine katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa sababu nchi ni Yetu,rasimali zilizopo ni zetu,madini ni yetu,mbuga za wanyama ni vya kwetu, hivyo ni muhimu Watanzania wakaamka sasa na kuonesha uzalendo wao halisi kama ambavyo Rais Dkt John Pombe Magufuli amekuwa akionesha kwa vitendo na kusisitiza suala zima la Uzalendo ndani ya nchi yetu.
 
"Sisi kama Wasanii, kwa moyo mmoja tumeamua kushikamana kwa pamoja na baraka zote tunazo kushikamana na kuiunga mkono kauli mbiu ya Rais Dkt Joh Pombe Magufuli ya UZALENDO KWANZA kuwa na harakati za kuifanya Tanzania yetu na Watanzania wenyewe kuwa Wazalendo kwa nchi yao",alisema Steve Nyerere na kuongeza kuwa kauli mbiu hiyo sio kwa ajili ya Dar Es Salaam tu bali,ni kwa ajili ya Tanzania nzima.

Mwenyekiti wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza Steven Mengele almaarufu kwa jina la kisanii Steven Nyerere akitoa ufafanuzi zaidi kuhusina na kampeni hiyo ya UZALENDO KWANZA mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar,kampeni hiyo inatarajia kuhamasishwa mikoa mbalimbali nchini .Pichani kushoto ni Msanii wa Filamu ni Misayo Ndumbagwe pamoja na Kemmy .

Baadhi ya Wasanii mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya UZALENDO KWANZA,itakayosambazwa nchi nzima kuhakikisha wananchi wanaelewa dhana nzima ya kuwa mzalendo na nchi yako.

Mkutano ukiendelea mapema leo wa uzinduzi wa kampeni ya UZALENDO KWANZA.

Msanii wa Filamu Wastara Juma akiwahimiza Watanzania kuwa WAZALENDO KWANZA katika mambo mbalimbali ikiwemo kuvithamini vya vyumbani,pia amewaomba Watanzania kuwaunga mkono Wasanii wao kwa kununu kazi zao zilizo halisi na halali ili kuhakikisha dhama nzima ya UZALENDO KWANZA inatimia.

Baadhi ya Wasanii wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa kampeni ya UZALENDO KWANZA,itakayopita mikoa mbalimbali kuwahamasisha wananchi kuwa Wazalendo na nchi yao na pia kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli katika suala zima la kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kimaendeleo.

No comments:

Post a Comment

Pages