September 07, 2017

Tigo yatoa simu 720 kwa washindi


Na Mwandishi Wetu
 
Dar es Salaam-Tanzania, Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, imetoa zawadi za simu papaso aina ya Tecno S1 kwa wateja wake 720 ambao wamejishindia simu hizo kupitia promosheni iliyofikia tamati ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi.

Akizungumza kwenye hafla ya kutoa zawadi kwa washindi 120 kutoka Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo Woinde Shisael alisema kwamba hii ni wiki ya nne na ya mwisho katika utoaji wa zawadi.

“Tofauti na promosheni nyingine   ambapo wateja wachache tu wanapata zawadi, Tigo inatoa simu moja ya Tecno S1, kila saa kwa masaa 24 kila siku ya wiki kwa muda wote wa kampeni hii ya kusisimua, kwa leo tumemalizia zoezi maana tumekabidhi simu zote 720,” alisema Shisael.

Kwa mujibu wa Shisael, promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe, Ujaziwe Zaidi inamuwezesha kila mteja wa Tigo kuwa na nafasi ya kujishindia simu anapoongeza salio, hii inaenda sambamba na kupata zawadi za papo hapo za kifurushi cha muda wa hewani, muda wa kuperuzi au kifurushi cha meseji kila anapoongeza salio.

“Tunafurahia kuona kwamba tumekuwa sehemu ya safari ya wateja wetu ambao wamejishindia simu za smartphone aina ya Tecno S1 ambao pia watafurahia mawasiliano ya bure ya simu kwa mwaka mmoja. 

Zawadi nyingine ambazo mteja alikuwa anaweza kujishindia ni pamoja na bonasi ya bure kwenye huduma ya sauti, data na ujumbe mfupi wa maneno SMS kulingana na matumizi ya mteja husika, "aliongeza Shisael.

Kwa mujibu wa Tigo, simu hizo zitawawezesha washindi kupata taarifa mabalimbali , kuchukua picha na pia kuzitumia katika matumizi mbalimbali.   

Wateja waliweza kushinda simu za mkononi kila saa kirahisi  kwa kuongeza muda wa maongezi  wa Tigo kupitia kadi za kukwangua, e-pin au TigoPesa, ambapo namba yao ya simu ilikuwa inaingizwa kwenye droo  ya  nafasi ya kushinda mojawapo ya simu za mkononi zilizoshindaniwa kila saa , ya kila siku kwa siku saba za wiki.

"Kama kawaida, Tigo inasikiliza na kuitikia   mahitaji ya wateja wake, na sasa tumewapatia zawadi kemkem kama njia mojawapo ya kuwashukuru kwa kuendelea kutumia bidhaa na huduma zetu bora. Nachukua fursa hii kuwashukuru wateja wote wa Tigo kwa kuwa pamoja nasi ambapo wengi wao wamejishindia zawadi mbalimbali,", aliongeza Shisael.

Kwa upande wake, Amon Mkude ambaye ni mkaazi wa Mbezi Msakuzi jijini Dar es Salaam, alisema kwamba hakuamini alipopigiwa simu kwamba kajishindia simu, “yaani sikuamini, nilidhani matapeli, ila nimeamini baada ya kupewa simu hii, nawashukuru sana Tigo kwa zawadi hii,” aliongeza Mkude.

 Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akimkabidhi simu aina ya Tecno S1 mmoja kati ya washindi 120 waliojishindia simu kwenye promosheni ya mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi, Sarah Lema, mkazi wa Tabata, jumla ya washindi 720 wamejishindia simu  nchi nzima . Hafla hiyo ilifanyika Duka la Tigo Manzese jijini Dar es Salaam

 Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akimkabidhi simu aina ya Tecno S1 mmoja kati ya washindi 120 waliojishindia simu kwenye promosheni ya mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi, Amour Haji, mkazi wa Mbagala, jumla ya washindi 720 wamejishindia simu  nchi nzima. Hafla hiyo ilifanyika Duka la Tigo Manzese jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages