NA KENNETH NGELESI,TUNDUMA
TIMU za soka za Morning Star na Mpira Pesa FC zote kutoka
mjini Tunduma Mkoani Songwe Oktoba Mosi mwaka huu zitakutana kwa ajili
ya kuwania Ubingwa wa kombe la Mbunge wa Jimbo hilo Frank Mwakajoka
‘Mwakajoka cup 2017’ utakao pigwa katika Uwanja wa Shule ya Msingi
Tuduma.
Akizungumza na Tanzania Daima jana Mjini Tunduma Kocha wa
timu ya Mpira Pesa FC, Maisha Kyando alisema kuwa amekuwa akiwangalia
wapinzani wanavyo cheza hawana jipya na kwa jinsi alivyo kiandaa kikosi
chake anaamini ubingwa kwa timu yake upo wazi.
‘Nawafahamu wapinzani wangu kikosi chao kiundwa na wazee
hawawezi kukimbizana na vijana wangu wa Mpira Pesa FC na jinsi nilivyo
jiandaa nina amini ubingwa ni wetu hawa Morning star hawana jipya nina
asilimia miamoja ya kubeba kombe vijana wanajua kuwa Jumapili ni kazi
hakuna ubishi ubingwa ni wetu’ alisema Kyando
Naye Rogadi Chuwa shabiki wa timu ya Mpira Pesa FC anasema
kuwa wao ni watu wa vita hivyo hakuna ubishi timu yao itachukua Ubingwa
wa Kombe la Mbunge
‘Sisi kama mpira pesa ni watu wa vita tumejipanga kushinda
kwani uwezo na sababu tunayo ya kushinda mchezo wa fainali na kuchukua
Tunduma inajua kuwa timu Mpira pesa FC ndiyo timu pekee inayoundwa na
vijana hata Mbunge mwenyewe anatajua kombe’ alisema Chuwa.
“Sisi tumeshashinda kwani vijana wetu wanacheza mpira wa
kitabuni mpira ulioenda shule hivyo, hiyo jumapili wapinzani wetu lazima
wakae’ alisema Chuwa shabiki wa Mpira Pesa FC
Mwenyekiti wa Timu ya Morning Star Boniface Mwakabanje
alisema kuwa timu yake italinyakua kombe hilo kwani klabu yake ina
mipango ya mpira kwa muda mrefu na hawajaufanya mchezo huo kama ajali.
Sisi ‘Morning Star, Mpira ni sehemu ya maisha yetu klabu
yetu inawacheza wenye nidhamu ya soka wamekaa pamoja kwa muda mrefu
wamejifunza mpira tofauti na timu zingine zimefanya kabumbu kama ajali
mfano ni hawa Mpira pesa FC wanacheza mpira baada ya wamesikia kuna
mashindano’ alisema Mwakabanje
‘Morning star ni timu pekee katika Mji wa Tunduma na Mkoa
wa Songwe kwa Ujumla na Tunduma unapozungumzia vilabu wa mpiga wa miguu
basi unaizungumzi timu hii ndiyo maana tunajiamini kubeba kombe’
Mwakabanje alisema ni maneno ya mdomoni kwani mpira ni
vitendo uwanjani kwani wanaitwa wazee ndiyo walioifikisha timu hiyo
fainali za michuano hiyo iliyonza mapema Agost mwaka huu kwa kushikisha
timu zaidi ya 30.
Alisema Monimng star ni timu pekee inayojua mpira katika
Mji wa Tunduma ndiyo maana katika michuano hiyo kulikuwa na timu zaidi
30 zilikiundwa vijana lakini kwa kuwa wamefanya mpira kama ajali
zilishindwa kufurukuta.
Mpira Pesa FC wametinga fainali hizo baada ya kuwafunga
Serengeti FC kwa jumla ya bao 1-0 huku Morning Star wakiwafurumusha bila
huruma Tunduma United bao 3-0 michezo yote ilipigwa katika dimba la
Shule ya Msingi Tunduma.
Michuano hiyo itafikia tamati Oktoba Mosi ambapo bingwa
ataondoka na kitita shi 500,000/,na kombe,mshindi wa pili sh.300,000/
,mshindi wa tatu sh.200,000/ mshindi wa nne sh.100,000/ na fungaji bora
ataondoka na kiatu. Mgeni rasmi anatazamiwa kuwa mbunge wa jimbo hilo
Frank Mwakajoka.
No comments:
Post a Comment