WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka
wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule mbalimbali nchini kusoma kwa bidii na
wasikubali kushawishika.
Pia Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka
sheria kali kwa wote watakaobainika kukatisha masomo ya watoto wa kike kwa
kuwapa ujauzito au kuwaozesha.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumatano,
Oktoba 04, 2017) wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya
Wasichana na WAMA Sharaf.
Shule ambayo ipo wilayani Lindi inamilikiwa
na Taasisi ya WAMA ambapo inasomesha watoto wa kike ambao ni yatima na
wanaotoka katika mazingira magumu.
Waziri Mkuu amewataka wanafunzi hao wa kike
kuhakikisha wanatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa bidii na hatimaye watimize
malengo yao.
Amesema ni vema wanafunzi hao wakatumia vizuri
fursa hiyo ya elimu wanayoipata shuleni hapo kwa kusoma kwa bidii na wafuate ratiba
itakayokuwa inapangwa.
“Nawasihi mtumie muda huu kusoma kwa bidii
ili muweke msingi imara ya kujenga maisha yenu ya baadae. Msikubali
kushawishika na kukatisha masomo yenu.”
Naye, Mwenyekiti wa
Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mbunge wa Kuteuliwa alisema
shule hiyo inasomesha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kutoka
mikoa yote nchini.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, OKTOBA 05, 2017.
No comments:
Post a Comment