HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 23, 2017

DC GONDWE AWATAKA WANANCHI WASICHOKE KUCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA AFYA

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akiongea na wananchi wa Kata ya Kwamgwe wakati akikabidhiwa zahanati iliyojengwa kwa hisani ya shirika la maendeleo la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na nguvu za wananchi, mkuu wa wilaya aliwaomba wananchi waendelee na moyo wa kujitokea katika kuchangia kazi za maendeleo ili kijiji kiweze kujikwamua kimaendeleo. (Picha na Kajunason/MMG).

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akimsaidia Diwani wa Kata ya Kwamgwe, Sharifa Abebe alipokuwa akitoa machozi ya shukrani kwa shirika la maendeleo la World Vision Tanzania kwa kuweza kushirikiana na wananchi kuwajengea jengo la zahanati lililoweza kugharimu shilingi milioni 190 ambapo wao World Vision Tanzania waliweza kutoa Milioni 100 na wao wananchi waliweza kujitoa kwa nguvu zao kwa thamani ya milioni 90. Hafla hiyo ilifanyika katika Kata ya Kwamgwe ambapo ndipo jengo hilo lilipojegwa.

Mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP wa World Vision Tanzania, Humphrey Bernard akisoma risala ya mradi wa ujenzi wa zahanati iliyojengwa katika Kata ya Kwamgwe ambapo aliwashukuru wananchi wa kata ya Kwamgwe kwa kuweza kujitoa kufanikisha ujenzi wa jengo la zahanati.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akikabidhiwa mikataba wa zahanati na mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP wa World Vision Tanzania, Humphrey Bernard (kushoto) ambao ndiyo waliojenga kwa kushirikiana na wananchi waliojitoa kwa hali na mali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni, William Makufwe akitoa ufafanuzi jinsi wananchi walivyoweza kujitoa ujenzi wa zahanati.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Dokta Credianus akitoa nasaha zake kwa wananchi wa Handeni waweze kujua umuhimu wa kuwekeza katika afya.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, akipokea zawadi ya kuku kutoka wa mwenyekiti wa kitongoji cha Migombani, Michungwani-Segera Bi. Amina Njama ambaye amekuwa msitari wa mbele katika uhamasishaji wa kukusanya matofali ili yaweze kusaidia katika ujenzi wa madarasa na zahanati.

Mkuu wa Wilaya akiwashukuru wananchi kwa moyo wao wa kujitolea katika maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Pages